Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Taasisi ya Benjamin Wiliam Mkapa BMF imekabidhi baiskeli 158 mabuti 25, na makoti ya mvua 25 na mabegi 150 vikiwa na thamani ya milioni 30 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajiri ya kuwawezesha wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutekeleza majukumu yao kwa urahisi zaidi .
Makabidhiano hayo yalifanyika hapo jana katika viwanja vya ofisi ya Mkoa wa Katavi ilipo katika Mtaa wa Ilembo na yalihudhuliwa na viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .
Afisa mradi wa Taasisi ya Benjamini Wilamu Mkapa TB na HIV DR David Mkali alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na wizara ya Afya Maendeleo na Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mpango wa Taifa wa kifua kikuu na ukoma pamoja na Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi inatekeleza mradi wa ukimwi na kifua kikuu chini ya Shirika ya shirika la Save the Children kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi ,kifua kikuu na Malaria .
Alisema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu katika Mikoa ya Rukwa , Katavi na Tabora unalenga kuisaidia Serikali kupunguza maambukizi ya kifua kikuu kwa silimia ishilini na tano na kupunguza vifo vitokanavyo na kifua kikuu kwa asilimia hamsini mpaka kufikia mwaka 2020.
Pamoja na hayo mradi mradi unalenga kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ,kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi ,kutokomeza unyanyapaaji na kuongeza upatikanaji wa urahisi huduma za ukimwi hasa upimaji wa VVU.
Dr Mkali alisema katika kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa Taasisi ya Mkapa imetowa mafunzo mbalimbali katika ngazi ya jamii ikiwemo mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 183 juu ya ubainishaji wa wagonjwa wa kifua kikuu ndani ya jamii.
Ili kufanikisha malengo ya mafunzo hayo Taasisi imekabidhi baiskeli 158,mabuti 25 na makoti ya mavua 25 na mabegi 150 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi zitakazo tumiwa na wahudumu wa Wilaya zote za Mkoa wa Katavi katika utekelezaji na ufuatiliaji wa majukumu yao ikiwemo ubainishaji na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kifua kikuu na ukimwi kwenye jamii husika .
Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Gabriel Chengula alisema Taasisi hiyo ya Benjamin Mkapo mbali ya kutowa vifaa hivyo pia wamefanya ukarabati katika Hospitali ya Inyonga na zahanati ya Simbwesa ili ziwe zinatowa huduma ya upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alieleza kuwa Serikali Serikali ya Tanzania imekuwa ikishirikiana na Taasisi ya Benjamini Mkapa katika kupambana na ukimwi na ushirikiano huo utaendelea.
Alisisitiza wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii watakao kuwa wamepewa vifaa hivyo wahakikishe wanavitunza na wanavitumia kwa matumizi yaliokusudiwa na si vinginevyo .
Nae mmoja wa afya wa ngazi ya jamii Salome John alieleza kuwa baiskeli na vifaa hivyo vitawasaidia kufika kwenye maeneo w anayofanyika kazi kwa haraka zaidi na wataweza kuwahudumia watu wengi kwa muda mfupi tofauti na awali .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment