Mlele
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele iliypo mkoani Katavi imemuhukumu mkazi wa
kijiji cha Mkuyuni – Majimoto , Roza John (39) kutumikia miaka 20
jela baada ya kukiri kosa la kumiliki nyara za Serikali zenye thamani
ya zaidi ya Sh milioni 1.5/-
Mshtakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 8
ya 2016 na makosa ya kupanga ambapo alikutwa akimiliki isivyo halali
ngozi tatu za mnyama aitwae kano na ngozi moja ya pakapori.
Akitoa hukumu hiyo , hakimu wa mahakama hiyo , Teotimus Swai alisema
kuwa licha ya mshtakiwa huyo kikiri kosa lake hilo mahakama hiyo
imelezimika kumpatia adhabu hiyo kali ili iwe fundisho sio kwake
tu bali pia kwa wengine wenye tabia kama yake.
Aliongeza kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu
cha 86(i) (2) na (ii) ya sheria ya hifadhi ya wanyamapori namba 5
ya 2009.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali , Jamila Mziray alieleza
mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Septemba 11
, 2016 katika kijiji cha Mkuyuni – Majimoto kilichopo katika wilaya
ya Mlele .
Mziray alidai kuwa siku hiyo ya tukio askari polisi walifanya
upekuzi nyumbani kwa mshtakiwa na kumkuta akiwa anamiki kinyume cha
sheria ngozi tatu za mnyama aitwae kano na ngozi moja ya pakapori
kwa pamoja zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 1.5/-
Mwisho
0 comments:
Post a Comment