Walter Mguluchuma Na Arine Temu .
Katavi .
Mtafaruku mkubwa umetokea katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda baada ya ndugu wa marehemu Mathias Madega kukabidhiwa mwili wa maiti ambao haukuwa wa ndugu yao baada ya watumishi wa afya kuuchukua mwili wa ndugu yao na kwenda kuuzika kwa madai kuwa haukuwa na ndugu .
Tukio hilo lililovutia hisia za watu wengi wa Mkoa wa Katavi lilitokea hapo juzi majira ya saa nane mchana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda .
Kat ka i tukio hilo siku hiyo ndugu wa marehemu Mathias walifika kwenye chumba cha kuhifdhi maiti kwa lengo la kuchukua mwili wa ndugu yao kwa ajiri ya mazishi yaliokuwa yamepangwa kufanyika siku hiyo ambae alikuwa amefariki siku mbili zilizopita .
Baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la George Madege akizungumza na wandishi wa Habari nje ya jengo la kuhifadhi maiti la Hospitali ya Manispaa ya Mpanda alieleza kuwa wao wamefika hapo kwenye chumba hicho kwa lengo la kuchukua mwili wa ndugu yao kwa ajiri ya mazishi na badala yake wameonyeshwa maiti ya mtu mwingine ambae mwili ulikuwa umeharibika vibaya huku mwili wa marehemu ndugu yao ukiwa haupo kwene chumba hicho..
Alisema kilichowashangaza wao ni kuonyeshwa mwili wa marehemu ambao sio wao na kuambiwa ndio mwili wa marehemu ndugu yao wakati maiti yetu ilikuwa na siku mbili na tukapewa mwili wa marehemu ambea hatumjuwi ambae alikuwa ameharibika sana .
Muhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali hiyo George Nsalamba alieleza kuwa siku hiyo yeye hakuwa zamu hivyo watumishi wa afya walipofika kuchukua maiti ambayo haikuwa ambayo haikuwa na ndugu kwa ajiri ya kwenda kuzika ndio waliokosea na badala yake walichukua mwili wa marehemu Mathias Mdega .
Alieleza kuwa ni kweli mwili wa marehemu waliopewa ndugu wa marehemu Mathias haukuwa wa kwao walipopewa ulikuwa umeharibika kutokana na kukaa kwenye chumba hicho cha maiti kwa muda mrefu .
Alisema mwili wa marehemu mathias umefukuliwa jana baada ya mahakama kutowa kibali cha kuufukua na tayari umewekwa katika chumba cha kuifadhi maiti kwa ajiri ya kubabidhiwa ndugu kwa mazishi na na mwili wa marehemu ulikuwa uzikwe na watumishi wa afya umechukuliwa na watumishi wa afya na kuzikwa jana katika makaburi ya Mwangaza kwa kutumia kaburi lile lile alilokuwa amezikwa Mathias .
Mazishi ya Mathias yamepangwa kufanyika leo katika makaburi ya Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda .
0 comments:
Post a Comment