Na Walter Mguluchuma Na Arine Temu Katavi . Mahakama
ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imemuhukumu kifungo cha maisha jela
mkazi wa Kijiji cha Kamsisi, tarafa ya Inyonga, Jilulu Lushinde (20)
baada ya baada kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita ambaye
ni wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Imalauduki
iliyopo wilayani humo.
Hukumu hiyo ilitolewa mahakamani hapo jana na hakimu wa mahakama ya wilaya ya Mlele, Teotimus Swai baada ya kuridhishwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande zote mbili za mashitaka na utetezi.
Awali, mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli alisema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo septemba 9, mwaka jana nyakati za jioni nyumbani kwa mtoto huyo anakoishi na wazazi wake.
Alisema siku ya tukio wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa wamekwenda harusini, mtoto huyo ambaye alibaki nyumbani kwao alivamiwa na kijana huyo na kubakwa na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri hali iliyosababisha kupiga kelele za kuomba msaada ndipo majirani walipojitokeza na kumuokoa.
Majirani hao walimkamata mtuhumiwa huyo na kutoa taarifa polisi kisha kumpeleka mtoto huyo kituo cha afya Inyonga ambako ilithibitishwa kwamba amefanyiwa kitendo hicho hivyo kupatiwa matibabu.
Lushinde alishitakiwa kwa mujibu kifungu cha sheria 130 (1) (2) (e) lakini alikana shitaka hilo, huku upande wa jamhuri ukiwa mashahidi wanne ambao walitoa ushahidi wao mahakamani hapo huku mtuhumiwa akijitetea mwenyewe.
Aidha, akitoa hukumu hiyo hakimu Swai alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo na shaka umemtia hatia kijana huyo, hivyo kwa kutumia kifungu cha 131 (1) sura ya 16 ya sheria iliyofanyia marekebisho 2002 mtuhumiwa anahukumiwa kwenda jela maisha.
Kwa mujibu wa sheria mtoto chini ya miaka kumi adhabu zake ni kifungo cha maisha jela, hivyo pamoja na mtuhumiwa kuiomba mahakama impunguzie adhabu lakini ombi lake hakusikilizwa.
Mwisho

Sumbawanga.Watu
watatu wote wa familia moja, wakazi wa kijiji cha Kipa tarafa ya
Mtowisa wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa wameuawa kwa kukatwa katwa na
mapanga na watu wasiojulikana kutokana na kile kinachodaiwa ni imani za
kishirikina.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, tukio hilo lilitokea nyakati za saa 8:45 usiku, feb 22 mwaka huu katika kijiji cha Mfinga kilichopo kata ya Mfinga wilayani humo, ambapo watu hao walivamiwa na kundi watu wasiojulikana na kuanza kushambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wao.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando aliwataja wanafamilia hao waliouawa kikatili kuwa ni Joachim Kayanda (60), Everina Mwanakatwe (47) na Emmanuel Kayanda (27) ambao wanaiwa kwenda Mfinga kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Kamanda Kyando alisema watu hao wakiwa wamekaa ndani ya nyumba yao wakijiandaa na kulala ghafla kundi la watu wasiojulikana walivamia nyumba yao kwa kuvunja mlango kisha kuingia ndani na kuanza kuwashambulia kwa kuwakatakata na mapanga wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, watu watano wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na watafikshwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Kamanda Kyando alitoa rai kwa wananchi kuachana imani potofu za za kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha kutokea kwa mauaji ya kujichulia sheria mkonono mara kwa mara.
Mwisho.

0 comments:
Post a Comment