Na Walter Mguluchuma
Katavi
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele iliypo katika mkoa wa Katavi
imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Tupido Ephance Seleman (42) kutumikia
miaka minne jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili kwa
kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinyume cha
sheria .
Aidha mshtakiwa huyo alitiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kukutwa na
lita tisa za pombe haramu maarufu ‘gongo’ baada ya kukiri kutenda
makosa hayo mawili huku akisema kuwa sare hiyo ya JWTZ alimnyang’anya
mtu mmoja aliyekunywa pombe hiyo haramu nyumbani kwake na kushindwa
kumlipa.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana kwa mara ya kwanza
ambapo alikiri kutenda makosa hayo mawili baada ya kusomewa mashataka
yake ..
“Nakiri kufanya makosa hayo lakini sare ya JWTZ nilimnyang’anya mteja
wangu aliyekunywa pombe aina ya gongo iliyopikwa nyumbani kwangu
baada ya kushindwa kunilipa “ alieleza
Hakimu wa mahakama hiyo ,Teotimus Swai licha ya mshtakiwa huyo kukiri
makosa yake amempatia adhabu hiyo kali ili iwe fundisho kwa wengine
wenye tabia kama zake.
Awali Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Baraka Hongoli alisema
kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo Januari , 29, mwaka huu,
Alisema siku hiyoya tukio askari polisi walipekuwa nyumba yake
kufuatia taarifa kuwa ni kinara wa kupika na kuuza pombe hiyo haramu
ndipo walipomkuta akiwa na sare moja ya JWTZ.
Mwendesha Mashtaka huyo aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali dhidi
ya mshtakiwa huyo ili iwe fundhisho kwa watu wengine ambao wamekuwa
wakimiliki sare za kijeshi kinyume cha sheria na kufanya uhalifu
wakiwa wamezivaa na kuchafua sifa ya jeshi hilo .
0 comments:
Post a Comment