Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Chama cha Msingi cha ushirika wa wakulima wa Tumbaku cha Mpanda Kati Mkoani Katavi kinatarajia kupanda miti milioni 7.5 zenye thamani ya Tshs 147,000,000 katika msimu wa kilimo wa 2017\ 2018.
Hayo yalisemwa hapo jana na Meneja wa chama cha Msingi cha wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati Rajabu Tembo wakati akitowa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama cha Msingi Mpanda Kati uliofanyika katika ukumbi wa Katavi Resort Mjini hapa .
Alisema chama hicho kimeisha omba mkopo Benki ya CRDB kiasi cha Dola 84,180 na tayati wameisha kubaliwa kwa ajiri ya shughuli ya kapanda miti katika msimu wa kilimo wa 2017\ 2018.
Alifafanua kuwa hari ya upandaji miti kwa wakulima wa tumbaku haukuwa wa kuridhisha katika msimu ulipita hari hari ambayo imesababisha kampuni ya Premium ipunguze kilo za kununua tumbaku kutoka kwenye chama hicho .
Rajabu aliwaeleza wajumbe wa mkutano mkuu huo kuwa Bodi ya Tumbaku imeisha weka sheria inayo elekeza kwa Makampuni yote yanayo nunua tumbaku hapa Nchini kununua t kilo za tumbaku kulingana na miti inayokuwa imepandwa kwenye chama husika .
Alisema msimu wa mwaka 2015 \ 2016 kampuni ya Premium ilinunua kiasi cha kilo za Tumbaku 1,600,000 na msimu huu wa 2016\ 2017 kampuni hiyo imeshusha kilo hadi kufikia kili 1,400,000 kutokana na chama hicho kutopanda miti inayolingana na kilo za tumbaku zinazotakiwa kuzalishwa .
Hivyo chama kimeweka mikakati mbalimbali ya kuacha kutegemea zao la tumbaku peke yake na badala yake wanatarajia kuanzisha mazao mchanganyiko ya mahindi na kalanga ..
Gerald Majura mjumbe wa mkutano huo alieleza kuwa ni vema kampuni ikaongeza kununua kilo za tumbaku ili kuwawezesha wakulima kukuza uchumi wao .
Alisema wakulima wamekuwa wakijitahidi kupanda miti ila wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mifugo kuharibu miti yao wanayokuwa wameipanda na kuwasababishia waonekane hawaja fikia malengo ya kupanda miti .
Charles Safisha mkulima wa chama hicho aliyaomba makampuni yanayotowa miti kwa ajiri ya kupanda wakulima wawe wanatowa miche ya mti matunda badala kupewa miche ya miti ya misongoma na misobali peke yake .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment