Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Madiwani wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekubaliana kuchangia kiasi cha Tshs 50,000 za posho yao ya mwezi zikatwe na zitumike kwa ajiri ya kuwapongeza walimu wa shule za Msingi kwa kuwa Manispaa hiyo imekuwa ya kwanza Kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo .
Uamuzi wa madiwani hao kutowa kiasi hicho cha fedha zinazotokana na posho yao mwezi walipitisha juzi kwene kikao cha Baraza la madiwani la Manispaa hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo .
Awali kabla ya kupitisha uamuzi huo Meya wa Manispaa Wily Mbogo aliambia Baraza hilo kuwa walimu wa shule za Msingi wa Manispaa hiyo wamefanya kazi kbwa na kuujengea heshima Mkoa wa Katavi kwa kuweza kuongoza Kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa mara ya tatu mfululizo katika Manispaa za hapa Nchini .
Mbogo alisema swala la kuwapongeza walimu kwa kazi yao nzuri wanayoifanya lisiwe la Manispaa peke yake bali liwe ni la Mkoa mzima kwani walimu hao ndio wamechangia Mkoa wa Katavi kuwa ni Mkoa wa pili kwa ufaulu wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana .
Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry kwa upande wake alieleza kuwa wao kama madiwani wa Manispaa hiyo wameridhia kuchangia kiasi hicho cha fedha kwa ajiri ya kutambua mchango wa walimu .
Alisema ni jambo la kujivunia kwa Manispaa hiyo kwani miaka ya nyuma watu walizowea kuona wanaongoza kwa ufaulu ni shule za kutoka mikoa ya kaskazini lakini mambo yamebadilika na wao wanaisoma namba kwa Mkoa wa Katavi
Diwani wa Kata ya Kawajense Pius Buzumale yeye aliwataka walimu kutoridhika na matokeo hayo na badala yake waongeze bidii katika kufundisha wanafunzi .
MWISHO
No comments:
Post a Comment