Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo ameliomba jeshi la Polisi Wilayani Mpanda kuwaondoa kwenye machimbo ya dhahabu madada poa waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza mili yao katika mtaa wa Fisi Mjini hapa ambao kwa sasa wamegundua mbinu mpya ya kwenda kufanya biashara hiyo kwenye baadhi ya machimbo ya dhahabu .
Mbogo alitowa ombi hilo kwa jeshi la polisi Wilayani Mpanda wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao cha Baraza la Madiwani wa manspaa hiyo kilichofanyika jana katika ukumbi wa manspaa ya Mpanda .
Alieleza kuwa pamoja na jihihada kubwa zilizofanywa na jeshi la polisi Wilayani hapa la kuwaondoa akina dada POA waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza mili yao akina dada hao wamebuni mbinu mpya tofauti na ile ya awali iliyokuwa imezoweleka .
Alisema badala ya kufanya bishara hiyo kwenye maeneo ya bar na kwenye kumbi za sitalehe sasa hivi wamehamia kwenye machimbo ya dhahabu yaliko katika maeneo ya Dilifu,Sikitiko na Kapanda .
Hivyo Mbogo aliliomba jeshi la polisi kufika kwenye maeneo hayo na kufanya utaratibu wa kuwaondoa kama walivyowaondoa katika Mtaa wa fisi .
Alieleza kuwa endapo madada POA hao wataachiwa kuendelea na bishara hiyo upo tena uwezekano wakati wa kipindi cha mavuno wakahama kwenye machimbo na kuhamia wanako vuna mazao na hasa ya mpunga .
Meya Mbogo alieleza baraza hilo kuwa kitendo hicho cha kufanyika kwa biashara ya kuuza miili yao akina dada kimepokelewa kwa mikono miwili na vijana na wazee wanaofanya kazi kwenye machimbo hayo .
Alisema watu hao wamekuwa wakifurahia kwa kile wanachokieleza kuwa kitendo cha akina dada poa kuhamia kwenye machimbo kumewapunguzia gharama ya kukodi pikipiki BODA BODA kwani hapo awali walikuwa wanalazika kuwafuata mjini katika Mtaa wa Fisi lakini sasa hivi wanapatikana hapo hapo .
Kwa upande wake mkuu wa jeshi OCD la polisi Wilaya ya Mpanda Veno Malesa ambae alikuwepo kwenye kikao hicho alieleza baraza hilo la madiwani kuwa swala hilo watalifanyia kazi mapewa iwezekanavyo.
Alieleza kuwa haoni sababu yoyote ambayo itakayo wafanya washindwe kuwaondoa akina dada hao wanaofanya biashara ya kuuza mili yao kama polisi waliweza kufanya kazi ya kuwaondoa katika mtaa wa Fisi kwani washindwe machimboni alisema ocd.
Mwaka jana aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima aliwaomba Madada poa waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza mili yao kwenye mtaa wa Fisi wafike ofisini kwake ili awapatie wataalamu watakao wapatia elimu ya ujasilimali ili waepukane na biashara hiyo
Nae Boda wa boda wa kwenye machimbo ya Dilifu Juma Hamisi akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu alieleza kuwa kwa sasa wateja wao waliokuwa wakiwachukua na kuwaleta Mpanda mjini wamepungua tokea kuhamia kwa akina dada hao kwenye machimbo
No comments:
Post a Comment