Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Jumla ya kesi 60 za tuhuma za mauwaji zimeshindwa kuanza kusiklizwa Mkoani Katavi na Mahakama kuu ya Sumbawanga kwa kipindi cha miaka miwili sasa kutokana na Mahakama kukosa fedha za kuendeshea kesi hizo .
Hayo yalisemwa hapo jana na kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Katavi Chiganga Ntengwa wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda
Alieleza kuwa zipo kesi 60 za mauwaji ambazo zimeshindwa kusikilizwa na Mahakama kuu ya Sumbawanga kwa kipindi cha miaka miwili sasa kutokana na ukosefu wa fedha ambapo kesi hizo huzikiliziwa Wilayani Mpanda .
Chiganga alieleza kuwa hari hiyo ya ukosefu wa fedha umesababisha Mahakama kushindwa kutowa haki kwa wakati kama ambavyo kauli mbiu ya mwaka huu inavyoeleza kuwa haki itolewe kwa wakati ili kuwezesha ukuaji wa uchumi .
Nae wakili wa ofisi ya mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Atlles Mlisa alieleza kuwa ucheleweshaji wa haki kwa wakati katika Mahakama umekuwa ni changamoto ya ukiaji wa kiuchumi kutokana na watu kutumia muda wao mwingi kufatilia kesi badala ya kufanya kazi .
Alieleza kuwa Mahakama mbalimbali zimekuwa zikishindwa kumaliza kesi kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali zinazozikabili mahakama hapa nchini .
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni rasilimali watu ambapo baadhi ya mahakama kuna tatizo la upungufu wa watumishi ,fedha pamoja na vitabu vya sheria .
Kwa upande wake mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja generali mstaafu Raphael Muhuga alizitaka Mahakama kutenda kazi muda wote kwa kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu ,jamii au uchumi .
Pia kutochelewesha haki bila sababu ya msingi ,kutoa fidia ipasavyo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa mengine na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge .
Mkuu huyo wa Mkoa aliwapongeza Mahakimu wakazi wawili wa Wilaya ya Mpanda kwa kutekekeza kwa ufanisi mpango wa kumaliza mashauri 27 yaliokuwa yamekaa kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka miwili ,katika kipindi kifupi cha miezi miwili tuu hivyo kuwafanya wahusika wa kesi hizo kuendelea na shughuli za ukuaji wa uchumi .
MWISHO
No comments:
Post a Comment