Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikimemo uchavu wa jengo lake kuwa livavuja hari ambayo imekuwa isababisha kuharishwa kwa kesi wakati wa mvua inapo nyesha wakati wa kipindi cha masika .
Changamoto hizo yalitolewa hapo jana na chama cha Mawakili wa kujitegemea Tanzania wa Mkoa wa Katavi wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliofanyika juzi katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda katika taarifa yao iliyosomwa na Mwenyekiti wao Patrick Mwakyusa mbele ya mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga.
Mwakyusa alieleza kuwa kumekuwa na changamoto wanayoipata ya uhailishwaji wa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda zinazosababishwa na uchavu wa jengo la Mahakama na kusababisha baadhi ya kesi haki kutotolewa kwa wakati hasa kipindi hiki cha masika .
Alisema wakati huu wa masika Hakimu ulazimika kuaharisha kesi mara mvua zinapo kuwa zimeanza kunyesha kutokana na jengo hilo la Mahakama kuwa linavuja hari ambayo imekuwa ikiwaletea usumbufu wao na wateja wao ,
Alitaja changamoto nyingine kwenye jengo hilo la kuwa halina chumba hata kimoja cha mawakili hari ambayo imekuwa ikiwawia vigumu kupata nafasi ya kuongea na wateja wao kabla ya kesi kuanza kusikilizwa .
Pia Mahakama hiyo haina chumba cha maabusu cha kuwaweka mahabusu a ambao wanakuwa wameletwa kutokea Magereza kwa ajri ya kusikilizwa kwa kesi.
Nae Wakili ofisi ya mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi Atiles Mlisa alieleza kuwa ofisi yao ya mwanasheria wa Serikali Mkoani hapa inakabiliwa na tatizo la rasilimali watu, fedha na vitabu vya sheria .
Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Katavi ambae pia ni Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa alisema kuwa jumla ya kesi 60 za tuhuma za mauwaji simeshindwa kusilizawa Mkoani Katavi kwa kipindi cha miaka miwili sasa kutokana na ukosefu wa fedha .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Gerelali Raphael Muhuga aliitaka Mahakama kutenda haki bila kujali hari ya mtu kijamii na kiuchumi na kutochelewesha haki bila sababu ya msingi .
Alitowa rai kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Katavi kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika ukarabati wa majengo ya Mahakama .
RC Muhuga aliwapongeza Mahakimu wakazi wawili wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na Odira Amwol kwa kutekeleza kwa ufanisi mpango wa kumaliza mashauri 27 yaliyokaa muda mrefu kwa zaidi ya miaka miwili ,katika kipindi kifupi cha miezi miwili tu hivyo kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za ukuaji wa uchumi ,
MWISHO
No comments:
Post a Comment