Na Walter Mguluchuma Na Arine Temu .
Katavi .
Idadi ya vifo vya mama vitokanavyo na uzazi zimeongezeka kutoka kutoka vifo 454 vya mwaka 2010 kati ya vizazi hai 100,000 na kufikia vifo 556 kwa mwaka 2015\216 kati ya vizazi hai laki moja ambao hupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi .
Hayo yalisemwa hapo jana na Afisa utawala wa taasisi ya utepe mweupe na uzazi salama Lyidia Kamwaga kwenye kikao cha wadau wa afya ya mama na mtoto wa Kanda ya Magharibi uliofanyia jana katika ukumbi wa Maji Mjini Mpanda na uliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi , Rukwa na Kigoma pamoja na waganga wakuu wa Mikoa hiyo na Mafisa Mipango .
Alieleza kuwa takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa wanawake 556 kati ya vizazi hai 100,000 TDHS 2015\2016 hupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi .
Alifafanua kuwa takwimu zilizotolewa mwaka 2010 zilikuwa zinaonyesha kuwa vifo 454 zilikuwa vitokea kati ya vizazi hai 100,000 .
Alisema katika utafiti uliofanywa na utepe mweupe katika Halmashauri 169 za hapa nchini waliweza kubaini Halmashauri 48 huwa azitengi fedha kwa ajiri ya dharula ya kupunguza vifo vya mama na mtoto mchanga .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga alisema tatizo la vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi linaaweza kupungua endapo Halmashauri zitatenga fedha za kutosha kwa ajiri ya kuokoa uhai wa mama na mtoto mchanga .
Alitowa mfano wa kituo cha Afya cha Mwese kilichopo katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wafanyakazi wa afya wamekuwa wakitowa huduma ya kuzalisha wajawazito kwa kutumia tochi za simu za mkononi kutoka na kituo hicho cha afya kutokuwa na huduma ya umeme kitu ambacho ni hatari kwa mama mjamzito .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Toxon Nzunda alieleza kuwa wajawazito wengi wamekuwa wakipoteza maisha wakati wa kujifungua kutoka na kujifungulia majumbani kwao .
Alitaja moja ya sababu inayowafanya wajawazito wajifungulie nyumbani ni kutokana na wahudumu wa afya kuwa na lugha mbaya kwa wajawazito wanapokuwa wamekwenda kiliniki hari ambayo imekuwa ikiwafanya waamue kujifungulia majumbani kwao na kukimbia hosiptalini .
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Hussein alieleza kuwa ili kufanikiwa katika kuokoa vifo vya mama na mtoto jamii na familia wanayonafasi kubwa ya kupunguza vifo hivyo .
Alisema kumekuwa na usimamizi mbovu wa kuwasimia wahudumu wa afya kwenye zahanati na kwenye vituo vya afya na matokeo yake kumekuwa kukitokea vifo vya akina mama na watoto ambavyo vingeweza kuzuilika .
MWISHO
No comments:
Post a Comment