Walter Mguluchuma Na Arine Temu.
Katavi .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga amezitaka HalmashaurI zote za Mikoa ya Katavi , Kigoma na Rukwa kutowa kipaumbele kwa kutenga fedha za kutosha kwa ajiri ya huduma za kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Wito huo aliutowa hapo jana wakati alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa afya ya mama na mtoto wa Kanda ya Magharibi uliowashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa hiyo waganga wakuu wa Mikoa , Maafisa Mipango wa Mkoa na waganga wakuu wa Wilaya uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji Mjini hapa .
Alisema Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea vifo vya mama vitokanavyo na uzazi wa mpango havija pungua kwa kiasi cha kuridhisha kutoka na sababu mbali mbali ikiwemo ya Halmashauri kutotenga fedha za fedha za kuokoa maisha ya mama na mtoto .
Alifafanua Mkoa wa Katavi ulifanya tathimini ya hali halisi ya huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto mchanga katika tathimini hiyo moja ya mambo yaliogundulika ili kuweza kuokoa vifo hivyo ni lazima kwenye kila kituo cha afya kuwe na chumba cha upasuaji , damu salama , nishati ya umeme na gari la wagonjwa .
Muhuga alieleza vifo vya akina mama na watoto vinaweza kupungua kwa asilimia 50 na pi a vifo hivyo vinaweza kuzuilika kama huduma kamili za uzazi za dharula zitapatikana katika vituo vya afya .
Alisema mpango wa serikali ni kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya hivyo one plain11 na imepanga kuwa kila kituo cha afya kiwezeshwe kwa kupatiwa wataalamu ili asilimia 50 ya vituo vya afya nchini viweze kutowa huduma za dharula za uzazi .
Afisa utawala wa Taasisi ya Utepe mweupe na uzazi salama Lyidia Kamwaga alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa wanawake 556 kati ya vizazi hai 100,000 TDHS 2015\ 2016 hupoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi .
Alisema kabla ya hapo takwimu za awali zilikuwa zikionyesha vifo ninavyo tokana na uzazi vilikuwa ni vifo 454 kati ya vizazi hai 100,000.
Mratibu wa afya wa huduma za afya ya uzazi na mtoto wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Josephina Joseph alieleza kuwa vifo vingi vya mama na mtoto vimekuwa vikisabishwa na uwezo mdogo wa wakunga walioko kwenye vituo vya afya na zahanati .
Katibu Tawala w Mkoa wa Rukwa Tioxon Nzunda alisema vifo vingi vimekuwa vikisababishwa na humbali wa maeneo wanayoishi watu na mahali panapo patikana huduma ya uzazi.
Alisema kwa Mkoa wa Rukwa idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi vipo zaidi katika Halmashauri ya Sumbawanga vijijini kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mbali na Hospitali ya Mkoa
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Hussein alishauri kuwa zitungwe sheria ndogo ndogo kwenye kila kijiji ili akina mama wanaojifungilia majumbani wawe wanatozwa faini .
MWISHO
No comments:
Post a Comment