.
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Katavi Peter Kabushi amewataka wafugaji amewataka wafugaji kukubali kutunza mazingira ili kukabiliana na utunzaji wa mazingira unaofanyika .
Wito huo aliutowa hapo juzi wakati alipokuwa akiwatutubia viongozi wa wafugaji wa kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Galden Mjini hapa .
Alisema wapo baadhi ya wafugaji ambao wamekuwa wakihamia kutoka kwenye Mikoa mbalimbali kiholela na wamekuwa waharibifu wakubwa wa mazingira .
Kapushi alieleza Wachungaji wa Mkoa wa Katavi wamekuwa na changamoto kubwa ya kutokuwepo maeneo ambayo yametengwa kwa ajiri ya wafugaji hari ambayo imekuwa ikisababisha wafugaji kulishia mifugo yao kwenye maeneo yasiyo kuwa yanasitahili .
Alisema ni vema Serikali ya Mkoa wa Katavi kabla ya kuwaondoa wafugaji kwenye maeneo waliovamia wasiwe wanaondolewa kwanza mpaka hapo watakapo kuwa wametengewa maeneo ya kupelekwa .
Alifafanua kuwa endapo watatengewa maeneo ya wafugaji wao watakuwa ni walinzi wazuri kwenye maeneo hayo kwa kuwadhibiti watu wanao hujumu mistu za kwenye Halmashauri kwani wao wafugaji huwa hawakati miti .
Alisema wamekuwa wakishangazwa na Halmashauri zilizopo katika Mkoa huu kwni wamekuwa wakiwatoza ushuru kwenye minada bila kujari kutenga maeneo kwa ajiri yakufugia mifugo .
Mustapha Mtesha mfugaji wa kutoka Kijiji cha Shankala alisema tatizo la migogoro ya wafugaji na wakulima imekuwa haimaliziki kutokana kutokuwepo kwa maeneo yaliotengwa kwa ajiri ya wafugaji .
Peter Maganga alieleza kuwa wafugaji wamekuwa wakikamatiwa mifugo yao na watumishi wa Halmashauri wa Idara ya Maliasili na wamekuwa wakitozwa fedha kiasi cha Tsh 50,000 kwa wafugaji wenye mifugo mingi wamekuwa wakitozwa fedha nyingi na wamekuwa wakiathirika kiuchumi kutokana na faini hizo .
John Budodi alililamikia kitendo cha askari wa Mali asili kuwatoza fedha za faini za mifugo bila kufuata utaratibu kwani wamekuwa wakiamuliwa kulipa faini wakiwa maporini huko huko badala ya kulipia banki.
MWISHO
No comments:
Post a Comment