Na Walter Mguluchuma .
Chama cha Wafugaji wa Mifugo cha Mkoa wa Katavi kimewataka wafugaji kuacha tabia na mazowea ya kupeleka fedha za hongo kwa watendaji wa Kata na vijiji pindi wanapokuwa wanapo hama na kuhamia kwenye eneo jingine .
Hayo yalibainishwa hapo jana kwenye kikao cha wafugaji wa kutoka katika Halmashauri za Manispaa ya Mpanda , Nsimbo , Mpimbwe na Mpanda kwa sasa Tanganyika katika kikao kiliofanyika katika ukumbi wa Galden Mjini hapa .
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji cha Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Tanganyika Peter Kabushi aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wafugaji kuwa na mazowea ya kupeleka fedha za kuwahonga watendaji wa Kata na wenyeviti wa vijiji hari ambayo imekuwa ikisababisha wafugaji kuhamia kiholela kwenye vijiji.
Alisema kitendo cha wafugaji kupeleka fedha kwa watendaji kimekuwa ni chanzo cha haki kutolewa pindi kunapokuwa kuwa na mggoro unapokuwa umetokea
Kabushi alieleza wafugaji wa Mkoa wa Katavi wamekuwa hawana maeneo ya kulishia mifugo yao hari ambayo imekuwa ikisabisha baadhi ya wafugaji kulishia mifugo yao ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenye mapori ya akiba hivyo i wanaiomba Serikali ya Mkoa kupitia Wilaya zake watenge maeneo kwa ajiri ya wafugaj kulishia mifugo .
Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa maliasili kuwachomea nyumba wafugaji na kuwasingizia kuwa ni majangili na hasa kwenye maeneo ya Kata ya Ugala .
Mfugaji Peter Maganga alieleza kuwa wafugaji wa Mkoa wa Katavi ni wapole mmo tafauti na wafugaji wa maeneo mengine kwani pamoja na matukio ya kuchomewa nyumba zao na mifugo yao kupigwa risasi hawaja wahi hata siku moja kurusha mishale kama wanavyofanya wafugaji wa maeneo mengine .
Kulwa Charles aliwalalamikia watumishi wa Maliasili kuwa wamekuwa wakiwatoza faini wafugaji wakiwa huko huko maporini na wamekuwa wakiwaandikia risti ambazo hazina uhalisia na malipo wanayokuwa wametowa alitowa mfano mfugaji anaweza kutakiwa kulipa milioni saba lakini kwenye risti wanamwandikia milioni tatu hivyo aliomba malipo yawe yanalipiwa Bank.
Pia alidai kumekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wanawake na watoto kwenye dolia zinazokuwa zinafanyika kwani wanapokuwa wamekosa wafugaji wanaume wamekuwa wakiwakamata wanawake na watoto na kuondoka nao .
Ramadhani Fumbo alisema yapo maeneo katika Kata ya Ugala ambayo yanauongozi wa Serikali katika vitongoji vitano lakini wamechomewa nyumba zao kitu ambacho kinachowashangaza waliweza kuruhusiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wa v itongoji kama kweli walikuwa kwenye maeneo ya tengefu ya mistu ya Kijiji.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando alilitolea ufafanuzi swala la wafugaji kulipia fedha za faini za mifugo inayokuwa ikpo ndani ya hifadhi za mistu wakiwa mapolini alisema malipo yote yanayozidi Tsh 2,000,0000 malipo yake yamekuwa yakifanyika Bank
Alisema inaelekeza mtu anaekamatwa na mifugo ikiwa ndani ya hifadhi za mistu hutozwa faini ya tsh 50,000 kwa kila mfugo mmoja wa ng-ombe
MWISHO
No comments:
Post a Comment