Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mkazi wa Kijiji cha Uzega Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani hapa Mashaka Kianga amejeruhiwa vibaya mguu wake wa kushoto hadi kuvunjika baada ya kupingwa na rungu na mke wake mkubwa wakati alipokuwa akiamua ugomvi wa wake zake mkubwa na mdogo waliokuwa wakipingana wakigombea mifuko mitupu ya mbolea ya Tumbaku .
Tukio hilo la mume kupingwa na rungu na mke wake mkubwa lilitokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi katika Kijiji cha Uzega .
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Abel Kalifumu alieleza kuwa kabla ya Mashaka kujeruhiwa na huyo mke wake mkubwa aliwakuta wake zake mkubwa na mdogo wakiwa wanapigana kwa ajiri ya kugombania mifuko mitupu ya mbolea ya Tumbaku aina ya NPK .
Alisema ugomvi wa wanawake hao ulianza baada ya mke mkubwa kumtaka mke mdogo ampatie mifuko mitupu ya kuwekea mbolea hata hivyo mke mdogo aliweza kumkatalia kumpatia mifuko hiyo na ndipo walipoanza ugomvi wa kupigana .
Kalifumu alieleza wakati wakiwa wanaendelea na ugomvi mume wao aliwakuta wakiwa bado wanaendelea kupigana hari ambayo ilimkasilisha mume wao Mashaka.
Ndipo Mashaka alichukua fimbo na kuanza kuwachalaza viboko kwa lengo la kuwaamua na ndipo mke mdogo alivyoona viboko vimemzidia aliamua kukimbia na kuwacha mke mkubwa. Katika eneo hilo .
Alisema kitendo hicho cha kuchalazwa fimbo kilimkasilisha mke mkubwa ambae aliamua kuingia kichakani na kurudi akiwa ameshika rungu na ndipo alipomshambulia mume wake kwa kumpiga mguuni hadi mguu wake wa kushoto ukavunjika .
Alisimulia kuwa majirani walikuwa karibu na eneo hilo walifika kwenye eneo hilo na kumchukua Mashaka na kumkimbiza katika zahanati ya Uzega ambako alipatiwa matibabu .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment