Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi limeiommmba Serikali imrudishe aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Esthom Chang-a ambae kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na aliyekuwa mwandisi wa Maji Resicipice Leo alihamishiwa Kigoma waruishwe Mpanda ili wakasimamie miradi ya maji ya zaidi ya shilingi milioni 150 ambazo waliwalipa makandarasi wawili wakati miradi ikiwa haija kamilika .
Maazimio ya kuiomba Serikali iliwarudishe viongozi hao yalitolewa hapo jana kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo kilichofanyika ukumbi wa idara ya maji .
Mwenyekiti wa Halmashauri Hamad Mapengo alilieleza baraza hilo la Madiwani kuwa kamati ya fedha na mipango ya Halmashauri hiyo imebaini kuwa miradi miwili ya ujenzi wa miradi ya maji katika shule za Sekondari ya Mpanda ndogo uliogharimu Tsh 72,000,000 na Kabungu Tsh 80.000.000 imeshindwa kukamilika kutokana na aliyekuwa mkurungezi wao Chang-a ambae kwa sasa ni DC wa Ukelewe pamoja na Mwandisi wa Maji Eng Leo kuwalipa wakandasa kiasi cha shilingi milioni 152 kwa miradi hiyo miwili wakati wakiwa hawaja kamilisha mradi i .
Alieleza kamati ya fedha na mipango ilipendekeza DC wa Ukelewe na Mwandisi Leo warudishwe na waje weleza ni kwani waliweza kulipa fedha za Halmashauri kwa wakandarasi ambao hawajamaliza kazi .
Hivyo kamati imependekeza watu hao wawili warudi ili wasimamie miradi hiyo na waikamilishe kulingana na fedha zilivyokuwa zimetengwa kwa ajiri ya miradi hiyo n ua warudishe fedha zote walizowalipa wakandasi hao .
Mapengo alieleza Halmashauri imeisha omba kwa Katibu Tawala wa Mkoa Katavi ili aweze kuandika barua ya kumtaka mwandisi Leo ambae kwa sasa yuko Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma aweze kurudishwa Mpanda .
Wakichagia mapendekezo hayo Diwani wa Kata ya Karema Maiko Kapata alilieleza baraza hilo kuwa kumekuwa na tabia ya wataalamu wa Halmashauri hiyo kuwapa majibu ya kuwadanganya madiwani .
Baada ya michingo mbalimbali iliyoolewa na wajumbe wa baraza hilo la madiwani lilipiisha azimio la kuwataka aliyekuwa Mkurugenzi wao kwa sasa DC wa Ukelewe na mwandisi Leo ambae kwa sasa ni mwandisi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma warudishwe Mpanda ili waje wasimamie miradi hiyo na kuikamiilisha kulingana na fedha zilizokuwa zimetengwa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando alilieleza Baraza hilo kuwa yeye kama kuwa yeye kama Mkuu wa Wilaya ya msimamizi wa halmashauri hiyo atahakikisha kila fedha ya halmashauri inapokuwa imepotea anachukua hatua mara moja .
0 comments:
Post a Comment