Na Walter Mhuluchuma .
Katavi .
Watu watatu wakazi wa Mtaa wa Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanashililiwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na Bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba za Nchi ya Uganda ikiwa na risasi 10 za SMG.
Kwa mijibu wa taarifa za Askari wa hifadhi ya Taifa ya Katavi watuhumiwa hao walikamatwa jana majira ya saa nane na nusu mchana katika eneo la Iku ndani ya Hifadhi ya Katavi .
Watuhumiwa hao kabla ya kukamatwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walikuwa wamepata taarifa za kuwa watuhmiwa hao wamepanga kwenda kufanya ujangili wa kuuwa wa Wanyama ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Kufutia taarifa hizo askari wa Hifadhi ya Katavi waliaandaa mtego wa kuwakamata na ndipo hapo jana waliweza kufanikiwa kuwakamata watuhimwa hao wakiwa ndani ya basi la kampuni ya SBS ambalo hufanya safari zake kutoka Mpanda kuelekea Mpimbwe Wilayani Mlele lenye Namba za usajiri T 223 ATW ambapo watuhmiwa walikamatwa wakiwa wanatokea Wilayani Mpanda.
Walisema baada ya kufanya upekuzi kwenye basi hilo ndipo walipoweza kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na bunduki aina ya SMG yenye Namba za usajiri za Nchi ya Uganda No UA 4461/1997 na risasi 10 za SMG zikiwa kwenye magazine wakiwa wamehifadhi ndani ya beji lao walilokuwa wakisafiria .
Baada ya kuwa wamewakamata watuhumiwa hao Askari wa Tanapa walikenda kufanya upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa mmoja wao kati ya hao watatu anae ishi katika Mtaa wa Uwanja wa ndege Manispaa ya aliyejulikana kwa jina moja la Mandago waliweza kumkuta na risasi tano za Bunduki ya SMG akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake na kufanya idadi ya risasi zilizokamatwa kwenye tukio hilo kuwa 15.
Kabla ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walikuwa kwenye dolia zao wiki mbili zilizopita walikuta tembo akiwa ameuwawa ndani ya Hifadhi ya Katavi ambae walimkuta akiwa hajatolewa meno yake na majangili ambao walikimbilia kichakani baada ya kuwaona askari wa Tanapa .
Ndipo baada ya kuuwawa kwa tembo huyo Tanapa walianza kufanya msako mkali kwa kutumia kikosi chake cha upelelezi na ndipo walipoweza kufanikiwa kuwakamata watuhmiwa hao ambao walikuwa wakielekea kufanya ujangili kwenye hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda amethibisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao watatu katika tukio hilo ambao mtuhumiwa mmoja katika yao anakesi nyingine kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za ujambazi na alikuwa nje kwa dhamana .
Alisema jeshi la polisi bado linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa mahojiano zaidi na mara baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili wakajibu tuhuma zinazo wakabili .
MWISHO
No comments:
Post a Comment