Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA Kanda ya Magharibi imetowa mafunzo kwa wajasiriamali wanaojihusisha na uchakataji wa vyakula na bidhaa nyongeza yenye lengo la kuwaongezea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokubalika katika masoko ya ndani na nje .
Mafunzo hayo ya siku moja yallyowashirikisha wajasiriamali wadogo wa kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi yalianyika jana katika ukumbi wa chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishina wa Polisi Paulo Chagonja.
Kaimu Meneja wa TFDA wa Kanda ya Magharibi Dkt Edga Mahundi alieleza kuwa kumekuw na malalamiko mengi kutoka kwa wajasiriamali wadogo na wakati kuwa wanashindwa kuingia katika soko la kitaifa na la Kimataifa la ushindani wa bidhaa .
Malalamiko hayo wamefanyiwa kazi na mamlaka ya chakula na dawa na ndio sasa imeamua kufanya mafunzo haya ya wajasiriamali ili waweze kupata elimu ya msingi ya uzalishaji wa bidhaa bora zitakazo weza kukidhi matakwa ya soko na hivyo kuongeza ushindani .
Dkt Mahundi alieleza kwa kufanya hivyo TFDA itashiriki kikamilifu katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya nchi yetu iwe ya uchumi wa kati wa viwanda na ndio maana mafunzo hayo yamefanyika kwa ushirikiano kati ya TFDA na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO
Alifafanua kuwa jukumu la TFDA ni kulinda afya ya jamii kwa kudhibithi ubora , usalama na ufanisi wa chakula na dawa TFDA imekuwa ikisajiri majengo ya uzalishaji wa bidhaa pamoja na usajiri wa bidhaa zinazozalishwa katika majengo hayo baada ya kujiridhisha zinakidhi vigezo vilivyowekwa kwa lengo la kumlinda mlaji .
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Paulo Chagonja aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa yatawaongezea tija wajasiriamali wadogo na kuwafanya waende kwenye ujasiriamali wa kati na baadaye wawe wajasiriamali wakubwa .
Alisema Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mkoa unaozalisha asali na karanga kwa wingi lakini unakabiliwa na changamoto ya masoko ya ndani na nje .
Alltaja baadhi ya sababu zinazochangia mazao hayo kukosa soko la ndani na nje ni kutokana na mazao hayo kuwauzwa yakiwa na viwango vidogo kutokana na kutoongezewa viwango .
Alisema hari hiyo imekuwa ikisababisha wafanya biashara wanao kuja kutoka nchi ya jirani na wakisha nunua bidhaa hizo na kuziboresha zinaonekana zietoka nchini kwao badala ya Mkoani Katavi .
Mwenyekiti wa wajasiriamali wadogo wa manispaa ya Mpanda Veronica Ntabagi alieleza mafunzoo hayo yatawawezesha kuwasaidia kupata bidhaa zenye ubora na kukidhi viwango .
MWISHO
No comments:
Post a Comment