Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Jeshi la Zimamato na uokoaji katika Mkoa wa Katavi linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi ikiwepo Boti kwenye Ziwa Tanganyika hari ambayo imekuwa ikisababisha kushindwa kufanya uakowaji kwa wakati.
Hayo yalisemwa hapo juzi kwenye taarifa ya kikosi cha zimamoto na uokoji cha Mkoa wa Katavi kwenye taarifa yao ya utendaji kazi iliyosomwa mbele ya Nabu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni wakati wa kikao chao na Nabu Wziri huyo kilichofanyika katika ofisi za jeshi hilo zilizopo katika Mtaa wa Mpanda Hotel.
Katika taarifa yao iliyosomwa na Mkaguzi msaidizi wa jeshi hilo Izraeli Kutika alieleza kuwa zimamoto Mkoani Katavi wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kutona na kuwepo kwa changamoto mbalimbali .
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kukosekana kwa Boti katika ziwa Tanganyika hari ambayo imekuwa ikisababisha washindwe kufanya uokoaji kwa wakati unaotakiwa .
Ukosefu wa vifaa vya kufanyi kazi pamoja na madawa hari ambayo inahatarisha usalama wa askari pindi wanapokuwa kwenye shughuli za uokoaji .
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni ukosefu wa gari kwani Mkoa mzima wa Katavi wanalo gari moja tuu lenye uwezo wa kujaza maji lita 1,500 ambalo pia ndio linalotumika kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda .
Izraeli alisema pia wanakabliwa na uchache wa watumishi kwani waliopo katika Mkoa wa Katavi wapo 36 na wote wanaishi katika manispaa ya Mpanda kutokana na kutokuwepo kwa ofisi za jeshi hilo katika Halmashauri nyingine za Mkoa huu.
Naibu Waziri Masauni aliwaagiza viongozi wa jeshi hilo waakikishe wanafungua ofisi katika Halmashauri zote zilizopo Mkoani Katavi.
Aliwasisitiza kuwa wahakikishe kunapokuwa kumetokea nyumba imeugua ni lazima wafike kwenye eneo hilo kwa wakati kwani kwenye maeneo ambako kuna gari la kuzimia moto halafu wakashindwa kufika yeye kama Naibu waziri hata waelewa .
Alisema Wizara itaendelea kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili Zima moto hivyo waendelee kufanya kazi wakati huu ambao changamoto zao zinaendelea kushughulikiwa .
Aidha amewagiza Idara ya uhamiaji wenye ofisi zao kwenye maeneo ya mikapani mwa nchi kutumia vizuri fedha zinazolipwa kutokana na malipo ya viza .
Alieza kuwa fedha hizo zinazotokana na malipo ya viza endapo zitatumika vizuri zitasaidia kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kwenye huduma ya jamii.
MWISHO
No comments:
Post a Comment