Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Mambo ya
ndani Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya siku moja .
aibu waziri wa Mambo ya
ndani Hamad Masauni akikagua gari la zimamoto la mkoa wa
Katavi ambalo ndilo gari pekee la zimamoto linatumiwa na Mkoa
wa Katavi katika matukio mbali mbali ya uzimaji moto pamoja na
kwa matumizi ya uwanja wa ndege
Naibu waziri wa mambo ya
ndani Hamad Masauni akikagua jengo la nyumba la kuishi askari
katika gereza la kilimo la Kalilankulukulu wakati wa ziara
yake ya siku moja Mkoani Katavi .
Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad
Masauni akiwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa
Wilaya ya Mpanda na wa Mkoa wa Katavi
Naibu
waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni akivishwa sikafu wakati
alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Katavi iliyopo katika
Mtaa wa Majengo A Picha na Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Serikali imedhamilia kutimiza lengo la mabadiliko ya utendaji kazi wa jeshi la zimamoto na uokoaji na kupunguza changamoto zinazo wakabili wafanyakazi wake.
Kauli hiyo iltolewa hapo juzi na Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na askari wa zimamoto kwenye ofisi zao zilizopo Mtaa wa Mpanda Hotel wakati wa ziara yake Mkoani Katavi.
Alisema Serikali inayo dhamira ya kweli ya kutimiza lengo la mabadiliko ya utendaji kazi wa jeshi la Zimamoto na uokoaji hapa nchini kwetu .
Alieleza kuwa Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazo zinazo likabili jeshi la zimamoto na itaendelea kuzitatua kadili inavyo wezekana hata kama sio kuzimaliza kabisa .
Aliwasisitiza kuwa pamoja na kuwpo kwa baadhi ya changamoto hizo ziwafanye wapunguze moyo wa kufanya kazi bali waendelee na kufanya kazi kwa nguvu zao zote wakati Serikali ikiwa inaendelea kuwatatulia changamoto zao .
Aliwaagiza waakikishe wanafubgua ofisi zao kwenye kila Halmashauri zilizopo katika Mkoa huu tofauti na ilivyo sasa ambapo ofisi ilipo ni moja tuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda tuu.
Masauni aliwahiza pia wawe wanawahi kufika kwenye matukio yanapokuwa yametokea kwa wakati kwa ajiri ya uokoaji kwa vile haoni sababu yoyote ambayo inaweza kuwafanya washindwe kufika kwa wakati wakati huku hakuna msongamano wa magari kama Dares salaam.
Kwa upande wake msoma taarifa ya utendaji kazi wa Zimamoto iliyosomwa kwa Nabu Waziri na Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Mkoani hapa Izraeli Kutika alieleza kuwa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana waliweza kukusanya kiasi cha Tsh 13,430,000 zilizotokana na ada ya ukaguzi wa kinga .
Alifafanua kuwa makusanyo hayo ya ada yalikusanywa katika Halmashauri moja ya Manispaa ya Mpanda kutokana na kutokuwepo kwa Ofisi kwenye Halmashauri nyingine hivyo hawakuza kwenda kukusnya ada hizo .
Izraeli alieleza kuwa jeshi hilo linakabliwa na uchache wa askari kwani walipo 36 kwa Mkoa mzima wa Katavi hawatoshi hari hiyo ndio imekuwa ikisababisha washindwe kufika kwenye maeneo mengine kwa wakati kwa ajiri ya oukoaji .
MWISHO
No comments:
Post a Comment