Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Hamad Masauni ameziagiza idara zote zilizopo chini ya Wizara ya ndani kununua sare zao na sare za wafungwa kwenye gereza la ukonga badala ya kununua sehemu nyi ngine kwa bei kubwa.
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara ya uhamiaji wa Mkoa wa Katavi katika ofisi zao zilizopo katika Mtaa wa Madukani .
Alisema zipotaatifa za kuwa baadhi ya wafungwa waliopo kwenye magereza ya Mkoa wa Katavi wanashindwa kutolewa nje ya gereza kutokana na kutokuwa na sare za wafungwa na matokeo yake wamekuwa wakikaa bure .
Alisisitiza kuwa kuanzia sasa sare zote za wafungwa zinununuliwe kwenye gereza la ukonga lilipo Dares salaam kwani huko wako mafundi wazuri na gharama zao sio kubwa .
Aliagiza kuwa idara zote zilizopo chini ya wizara ya Mambo ya ndani katika Mkoa wa Katavi kuhakikisha kuanzia sasa sare zao wanazinunua kwenye gereza la Ukonga na sikwingineko .
Alisema Serikali imeisha amua kutumia lasilimali zake zilizopo hapa nchini miongoni mwa rasimali watu ni wafungwa waliopo kwenye mageeza mbalimbali .
Masauni alieleza wameisha amua kuwatumia wafungwa walioko magerezani kwa ajiri ya kufanya shughuli mbambali kwenye taasisi za Serikali kwa kujenga majengo na kufyatua matofali .
Na kutaiwezesha Serikali kupunguza gharama za ujenzi wa majengo yake na fedha zitakazo ukolewa zitatumika kufanya shughuli nyingine za akimaeneleo alisema Masauni.
MWISHO
No comments:
Post a Comment