Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Hamad Masauni amewatahadharisha Raia wapya wa Tanzania na wakimbizi wanaoishi katika makazi ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kuwa Serikali itawachukulia hatua wale wote ambao wanafanya kuingiza silaha ,kufanya vitendo vya ujambazi na ujangili .
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nduw Makazi ya wambizi ya Katumbai.
Alisema Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria wote watakaobainika kufanya hivyo kwani kupewa uraia wa Tanzania sio sababu ya wao kufanya vitendo hivyo .
Masauni alisema taarifa zilizopo Serikalini zinaonyesha kuwa baadhi yao waliopewa Urai na wakimbi zi wanaoishi kwenye Makazi hayo sio waaminifu na wamekuwa wakifanya vitendo vya uharifu.
Alisisitiza kwamba katu hatuta sita wala kuwavumilia watu wa aina hiyo kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuruhusu vitendo hivyo kufanyika katika ardhi ya Tanzania .
Alisema Serikali ipo tayari kuchukua maamuzi magumu kwa wale wote waliopewa uraia wa Tanzania endapo watabainika kufanya vitendo hivyo kauli hii ambayo maamuzi iliwatia hofu baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye mkutano huo kwa kuhofia kufutiwa uraia wao.
Aliwataka waache tabia wanayoifanya ya kubaguana kwani wanapaswa watambue kuwa wtu wote ni ndugu moja na wao ndokane na kuwa na moyo mbili za nchi ya Burundi na Tanzania .
Alieleza kuwa kumekuwepo na hali ya kubaguana kwa watu wanao ishi kwenye makazi hayo hari ambayo imefikia mahali hadi watu wananyimwa kuchota maji kwenye bomba na visima jambo hilo sio zuri kabisa na ni jambo la aibu wala sio utamaduni wetu .
Alisema Tanzania kuna amani kwa kuwa watu hawabaguani na hivyo hivyo hawatarajii uona mtu yoyote anatutenganisha kwa misingi ya ukabila ,dina wala rangi .
Alifafanua kuwa wananchi wa Katumba ni raia wa Burundi na majirani kiasili ni ndugu wa damu hivyo watambue kuwa katumba ni kwao na Tanzania inafanya kazi kubwa ya kufanya majirani zetu wanakuwa salama.
Nae Diwani wa Kata ya Katumba Seneta Baraka alieleza kuwa watu kufanya vitendo vya uharifu ni akutokani na mtu kuwa raia wa kutoka Nchi ya Burundi bali ni tabia ya mtu mwenyewe.
MWISHO
No comments:
Post a Comment