Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Kumekuwa na taarifa za upotoshwaji kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula hapa nchini
ambapo hali hiyo inasababisha wananchi kukata tamaa ya kuendelea
kufanya kazi hasa ya kilimo na badala yake kubaki kuilalamikia Serikali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wameihakikishia
nchi kuwa Tanzania iko salama na chakula kipo cha kutosha hivyo
wananchi wasisikilize watu wengine ambao wana nia ya kuupotosha Umma.
Akizungumza
baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa alisema nchi
haijakumbwa na baa la njaa na aliwataka Watanzania kutosikiliza kampeni
za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara kuhusu hali ya
chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha
bei za vyakula.
Nae
Waziri Tizeba alisema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya
kuridhisha na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazodai kuwa hali ya
chakula ni mbaya.
Tatizo
kubwa lililopo ambalo linawachanganya Watanzania wengi ni kuchanganya
kati ya ukame na ukosefu wa chakula, wanaamini kuwa nchi ikiwa na ukame
lazima kutakuwa na njaa lakini si kweli kuwa vitu hivi vinaendana.
Nchi
yaweza kuwa imekumbwa na janga la ukame lakini isiwe na janga la njaa
kwani kuna mazao ambayo yanastahimili ukame ambayo yanaweza yakalimwa na
kutoa mazao yatakayowawezesha wananchi kujipatia chakula pamoja na
kuuza ziada ya chakula hicho ili kupata fedha za kujikimu.
Mazao
mengi ya jamii ya nafaka yana uwezo mkubwa wa kustahimili ukame, mazao
hayo ni pamoja na mihogo, viazi na mahindi, hivyo wananchi wanapaswa
kwenda na wakati kama hali ya nchi ni ya ukame basi walime mazao
yanayoendana na wakati huo na si vinginevyo.
Tusiwe
wabishi kung’ang’ania kufanya kilimo ambacho tumekizoea kwani hali ya
hewa ama tabianchi kubadilika ni jambo lisiloepukika na linatokea muda
wowote, hakuna wa kulaumiwa kuhusu mabadiliko hayo zaidi ya wananchi
wenyewe kukubali mabadiliko hayo na kwenda sawa nayo.
Pia
tunashauriwa kutumia mbegu zitakazokomaa mapema ili kupata mavuno kwa
haraka na kwa wingi pamoja na kutumia mazao wanayoyapata kwa uangalifu
na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya.
Serikali pia inajitahidi kwa hali na mali kuwasaidia wananchi kuwa na maisha bora ambapo pamoja
na kuwepo kwa hali nzuri ya chakula, Serikali kupitia Wakala wa Taifa
wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kuweka akiba ya chakula kwa
kununua jumla ya tani 62,087.997 za mahindi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na chakula cha kutosha,
Wizara
kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, FAO, TFNC pamoja na
wadau wengine wanaendelea kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula
na lishe nchini ambayo inatarajiwa kukamilika Januari 28 mwaka 2017 na
itazihusisha Halmashauri 55, tathmini hiyo itaiwezesha Serikali kupata
taarifa za uhakika zaidi kuhusu hali ya chakula na lishe nchini.
Hivyo
wananchi wanatakiwa wafanye kazi, wasifate maneno ya watu yenye lengo
la kupotosha jamii bali wawasikilize viongozi wao ambao waliwachagua
wakiamini kuwa watawaongoza na watawatatulia matatizo yao.
No comments:
Post a Comment