Wednesday, February 1, 2017

HIFADHI ZA TAIFA NA MAPORI YA AKIBA ZAKABLIWA NA CHANGAMOTO ZA UJANGILI NA MIFUGO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Askari wa  TANAPA  na  wamamlaka ya  Ngorongoro  na  TAWA  wakipita  mbele ya    Katibu mkuu wa  Wizara ya Maliasili na  Utalii  wakati wa   kumaliza   mafunzo ya   Askari  hao waliomaliza mafunzo ya  mwezi mmoja   katika    kituo  cha  mafunzo  cha  Askari wa   wanyama  pori  cha   Mlele   Mkoa wa  Katavi 
   PICHA  NA  Walter  Mguluchuma
   Na  Walter  Mguluchuma 
  Katavi .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jnerali Gaudence Milanzi amesema kuwa Hifadhi za  Taifa na    mapori ya  akiba   yanakabiliwa   na     changamoto   nyingi    za  uwindaji  wa  wanyama  wakubwa   kama Tembo ,    Faru,  kwa  ajili  ya pembe   na  vipusa   pamoja  na    uingizwaji  wa  mifugo   ndan i ya  Hifadhi hali ambayo inathiri ustawi wa hifadhi na mapori.
Kauli  hiyo    ilitolewa  jana          wakati    akifunga   mafunzo ya   wahitimu   wa    mafunzo ya   uongozi  kwa   askari 113  waandamizi  wa  Tanapa ,Mamlaka ya    Hifadhi  ya  Ngorongoro  NCAA   na  TAWA    yaliyofanyika   katika  kituo  cha  mafunzo    cha  Mlele  Mkoani   Katavi.
 Alisema  kuwa  kwa   sasa   hifadhi  zetu  pamoja  na  mapori      yote   yanakabiliwa  na   changamoto   nyingi   sana   zikiwemo   uwindaji  wa  wanyama   wakubwa   kama   Tembo    na  Faru  kwa  ajili   ya pembe   na  vipusa ,uingizwaji wa  mifugo   hifadhini  pamoja  na nyingine  nyingi .
  Milanzi  alieleza kuwa  kwa  sasa    Tanzania   imekubwa  na   changamoto  kubwa  ya  ujangili  wa kutumia   silaha   za  aina  mbalimbali  za  moto   na  hasa   zile za  kivita   hali   inayoenda  sambamba  na  matukio  ya  kigaidi   yanayotokea   maeneo  mbalimbali   duniani  na  mengine  ya  hivi  karibuni  ya   unyanganyi  wa  kutumia  silaha   hapa  kwetu   Tanzania .
  Toka   taasisi   za     Hifadhi   TANAPA    na  Ngorongoro    zianzishwe   zimekuwa  kwenye  mfumo  wa  utendaji  kazi  wa  kiraia   ambao  Wizara   imeona   umeshindwa   kutatua    changamoto  na  matatizo  mbalimbali   yanayokabili   uhifadhi  kwa  ujumla .
Alisema  Wizara  kwa  kutambua  hilo  ndio  maana    inabadilisha  mfumo  wa utendaji  kazi  wa  taasisi  hizo  kutoka   mfumo wa  kiraia  na  kuwa    jeshi  usu  kwa  dhamira   sahihi  na kwa   umoja    Wizara ya  Maliasili  na  Utalii  inaamini    changamoto   za   ujangili na uingizaji wa  mifugo  ndani ya  Hifadhi   zitafikia    mwisho.
 Alisitiza  kuwa  Serikali   haipendi migogoro na   wafugaji  na wala   sio  nia ya Serikali  kuona  watu wake  wanakufa .
Aliwataka  watumishi wa  taasisi hiyo kutokumia  nguvu kubwa  pale  ambapo   hapa  sitahili  hivyo  watumie  silaha wanazokuwa  wamepewa kwa  waledi  na  wazitumie  pale  inapo  bidi  na   wananchi  nao  wanapaswa  kutii  na  kufuata  sheria za  uhifadhi  kama  ambavyo  zinaelekeza  na waache  tabia  ya  kuwapiga  askari.
Naibu    mhifadhi  mkuu wa  TANAPA  Mtango  Mtaiko  alieleza  kuwa  mafunzo kama  hayo yatakuwa  yakifanyika mara  kwa  mara  kwenye  chuo  hicho ili kuwafanya  wasiwe wa kizamani  ili  kukabiliana   na  mbinu  mpya  za  majangili .
Naibu  Mhifadhi  wa  mamlaka ya  Ngorongoro   Maulusu  Msuha  alisema  mfumo  mzima wa  utendaji kazi unabadilika  hivyo  watumishi  nao   wabadilike   na waende   na  wakati  na  watumishi wote  pamoja  na  maafisa  wao  lazima   wapate  mafunzo ya  kuwatowa  kwenye  mfumo wa  kiraia  na   kuelekea  jeshi usu.
Mwakilishi wa  Mkurugenzi  mkuu  wa   mamalaka  ya  usimamizi  wa  wanyama  pori  aliwataka  watumishi wa taasisi hizo  wazingatie  sheria  na  kanuni  wanapo  kuwa wakiwakamata  watuhumiwa  ili kuepukana na  kesi  na pia  wafanye  kazi kwa  masilahi ya  Taifa  na wazingatie  tija     na  usalama wa  Taifa .

No comments:

Post a Comment