Monday, August 15, 2016

WANDISHI WATAKIWA KUSHIRIKI MAFUNZO YA KIJESHI YANAYOTOLEWA NA TANAPA

 
Na  Walter  Mguluchuma
      Katavi
     Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii  imewahimiza  wanahabari  kujiunga  na  mafunzo  ya kijeshi  yanayotolwa  na  shirika  la  Hifadhi Taifa  TANAPA  ili waweze  kuzielewa  changamoto  zake   badala ya kuandika na kutangaza    habari  zake tuu.
  Ushawishi   huo  ulitolewa    na  Katibu  mkuu wa  Wizara    hiyo   Meja  Jenarali   Gaudensi   Milanzi  wakati  akifunga   mafunzo  ya  Askari  wa Tanapa  na uhifadhi wa  Ngorongoro .
  Alisema  Tanapa  ipo  katika  kubadili  mfumo  wa utendaji  wa kazi  kutoka   ule wa  kiraia  kuwa  jeshi Usu   Paramlltary System ili  kukabiliana  na  tatizo    sugu  la ujangili  wa  wanyama   mistu  na  rasilimali   nyngine za  Nchi .
 Badala ya wandishi wa  habari  kuja kila  siku  huku  na kuandika   na kutangaza   habari  zetu  sasa   nyinyi tunawaalika  mjiunge  nasi   katika  mafunzo  ya kijeshi  hii itasaidia  sana  kutambua  changamoto   zetu  pia  kujenga   afya  ya  akili na   mwili  kwa kufanya  mazoezi .
 Akizungumza    alisema    maombi ya  Tanapa  kutaka   kubadilishwa  na kuendeshwa  kwa  sheria  za Kijeshi  ni  yamsingi  katika  kipindi  hiki   ambacho   Tanzania  inakabiliwa  na  tatizo  sugu  la  ujangili wa  wanyama pori .
  Ufungaji wa  mafunzo  hayo  ulifanyika  juzi   katika   kambi ya  Mlele   Mkoa wa  Katavi   ndani ya   Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi   ambapo  Mameneja  10 na  Askari  58 kutoka  Tanapa  na  uhifadhi wa  Ngorongoro  walihitimi  mafunzo  hayo ya  mwezi  mmoja .
 Naamini  pasipo  shaka    mafunzo  yatawasaidia  kuimarisha   nidhamu  kipindi  hiki  tunachojiandaa  kuingia  katika  mfumo  tarajiwa  wa kiutendaji  wa jeshi Usu .
Kwa  sasa  uhifadhi  unakabiliwa na  changamoto  kubwa   ya ujangili  hususani  wa Tembo  na  Faru  kuporomoka kwa maadili  kwa  baadhi ya  askari wa Tanapa  na uingizwaji wa  mifugo  Hifadhini  alisema  Meja  Jenerali  Milanzi .
 Alisema  sheria ya uanzishwaji wa  jeshi Usu  ilichelewa kutekelezwa  ambapo  ikiendelea  kucheleweshwa  itasababisha  kuchelewa   kupatikana kwa  vitendea  kazi  vya kisasa .
Hata  hivyo  aliwakaka  Askari  hao  pamoja  na  Menejimenti  kufanya maandalizi ya kutosha  kwa misingi ya kuwa na  sheria  itayopitishwa  baadhi ya  mabadilio  na uendeshaji  kwa  utaratibu  wa  kama  majeshi  mengine
 Awali   akiwasilisha  maombi   hayo     Mkurugenzi  Mkuu  wa  Tanapa Allan  Kijazi   alisema   shirika   hilo   baada ya  kutafakari kwa kina  kwa kutumia watalamu wake wa ndani  walibaini umuhimu wa  askari wao  kutumia  sheria za kijeshi  kutokana  na  changamoto  ya sasa  katika   maswala ya uhifadhi .
  Nae  Meneja wa    mapori ya   akiba ya  Rukwa   Lwafi  Joseph  Mwang-ombe  alisema   kambi  hiyo ya  Mlele   inakabiliwa  na   changamoto  kadhaa  ikiwemo  uwanja wa  ndege kutokalabatiwa  kwa wakati , uchakavu  wa majengo  na miundo  mbinu ya  maji  pamoja na  mawasiliano ya  simu .
Wakiongea  na  gazeti  hili wandishi wa  Habari   Alslaji  Mvungi w  ITV  Ar usha , Joshua  Joel  Itv  Rukwa  Adolfu  Mbata  Tbc  Katavi ,Bibada  Erenest   Azamu  Katavi  na  Pety  Siame  Habari  Leo  Rukwa  walisema kuwa  wao  wako   tayari kujiunga  na  mafunzo  hayo  pindi watakapo  kuwa wamehitajika kufanya  mafunzo  hayo.

No comments:

Post a Comment