Na Walter Mguluchuma , Katavi .
WIZARA ya Maliasili na Utalii imeridhia maombi ya Shirika la Hifadhi
la Taifa (TANAPA) kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia
na kuwa jeshi usu ili kukabiliana na tatizo sugu la ujangili wa
wanyamapori.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya askari na wahifadhi wa shirika
hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi
alisema maombi ya shirika hilo kutaka kubadilishwa na kuendeshwa kwa
sheria za kijeshi ni ya msingi katika kipindi hiki ambacho Tanzania
inakabiliwa na tatizo sugu la ujangili wa wanyamapori.
Ufungaji wa mafunzo hayo ulifanyika jana katika kambi ya Mlele ndani
ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi mkoani Katavi ambako mameneja wahifadhi
10 na askari 58 walihitimu mafunzo ya kijeshi ya mwezi mmoja
“Naamini pasipo kutia shaka mafunzo haya yatasaidia kuimarisha
nidhamu kipindi hiki tunchojiandaa kuingia katika mfumo tarajiwa wa
kiutendaji wa Jeshi Usu (paramilitary system)
Kwa sasa uhifadhi unakabiliwa na changamoto kubwa ya ujangili,hususan
tembo na faru kuporomoka kwa maadili ya askari na uingizaji wa mifugo
hifadhini,” alisema Meja Jenerali Milanzi.
Hata hivyo, aliwataka askari hao pamoja na Menejimenti ya Tanapa
kufanya maandalizi ya kutosha kwa msingi kuwa sheria itakapopitishwa
baadhi ya mambo yatabadilika na kuendeshwa kwa mujibu wa taratibu za
kijeshi kwa ilivyo kwa majeshi mengine nchini.
Awali akiwasilisha maombi hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan
Kijazi alisema shirika hilo baada ya kutafakari kwa kina wakitumia
wataalamu wa ndani ya shirika walibaini umuhimu wa askari wao kutumia
sheria za kijeshi kutokana na changamoto ya sasa ya katika masuala ya
uhifadhi.
Alisema shirika limejipanga kuhakikisha linakabiliana na hari ya ujangili katika maeneo yote .
Naye Meneja wa Pori la Akiba la Rukw / Lwafi , Joseph Mwang’ombe
alisema kuwa kambi hiyo ya mafunzo inakabiliwa na changamoto kadhaa
ikiwemo uwanja wa ndege kutokarabatiwa kwa wakati , uchakavu wa
majengo na miundombinu ya maji na gharma kubwa ya uendeshaji .
No comments:
Post a Comment