Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu blog
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Mchemba ameyaagiza Majeshi ya Polisi na Magereza kuacha kujenga nyumba za makazi ya Askari zenye ramani ya Kikoloni na badala yake wajenge makazi ya Askari yenye ramani za kisasa .
Mwigulu Mchembe alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na askar wa Mkoa wa Katavi wa kutoka majeshi ya polisi , Magereza , Uhamiaji na Zimamoto kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini hapa.
Alisema wakati Wizara ya mambo ya ndani inatengeneza Jeshi la kisasa ni vema na askari naowakajengewa makazi yao na yakawa ya kisasa ili yaendane na jeshi hilo kuliko ilivyo sasa ambapo makazi yao yamekuwa yakijengwa kwa ramani za toka wakati wa Wakoloni .
Mchemba alieleza askari wamekuwa wakishindwa hata kutembelewa na wazazi wao kutokana na aina ya makazi ya nyumba wanazoishi .
Hivyo ni vema ramani za makazi ya askari kuanzia sasa Askari wajengewe nyumba ambazo zitawaruhusu wazazi wao kuwatembea
Alisema tatizo la upungufu w nyumba za askari hapa nchini ni kubwa na lisipotatuliwa linaweza kupunguza hari ya utendaji wao wa kazi kwani mchana ukiingia kwenye nyumba hizo ni joto kama tanuli la moto na usiku ni baridi
Alifafanua kuwa Mikoa mpya na Wilaya mpya zinanafasi kubwa ya kujenga vizuri makazi ya nyumba za kuishi askari kuliko ilivyo kwa Mikoa ya zamani na Wilaya za zamani kwani wanayo maeneo makubwa .
Aliyataka majeshi hayo kuanza kujenga makazi kwa kutumia rasilimali walizo nazo badala ya kukaa wanasubilia bajeti ya kutoka serikalini .
Pia Waziri Mchembe aliwaeleza askari hao kuwa Polisi wanayofurusa kubwa ya kuwasaidia watu mbalimbali wanaokuwa wameonewa .
Aidha alilipongeza jeshi la polisi Mkoani Katavi kwa kuulinda Mkoa huo na kuufanya kuwa salama na pia kwa jitihada zao za kuwakamata watu wanao hujumu nyara za Serikali .
No comments:
Post a Comment