Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu Blog.
Chama cha Walimu Wilaya ya Mpanda CWT kimewapatia zawadi wastaafu wake walimu sita waliostafu kuanzia Januari hadi June bati 120 zenye thamani ya shilingi milioni tatu ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango waliotoa katika utumishi wao wa kazi ya elimu.
Katika zawadi hizo za mkono wa kwa heri kwa walimu hao sita wa kutoka Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kila mmoja alipatiwa bati 20.
Zawadi hizo walikabidhiwa hapo juzi katika sherehe za kuwapongeza walimu hao zilizofanyika katika ukumbi wa Chekechea wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishina Paulo Chagonja aliyewakilishwa kwa niaba yake na Afisa Elimu wa Mkoa wa Katavi Erenesti Hinju.
Katika hutuba yake aliyoitowa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kabla ya kukabidhi zawadi hizo aliwataka walimu wanaokuwa wanastafu kuwacha tabia yao ya maisha waliokuwa nayo sio wana badilika na kukimbia familia zao pindi wapatapo mafao yao .
Alisema wastafu wengi hasa walimu wamekuwa na tabia ya kuchukua mikopo kwenye taasisi za Benki binafsi na kwa wafanya biashara mikopo yenye liba kubwa ambapo wakekuwa wakikopeshwa milioni 20 na wao wanalipa milioni 40 kitu ambacho kimewaathiri wastafu wengi hivyo ni vema wajiepushe na liba za namna hiyo.
Imekuwa ni aibu kwa tabia ilijengeka kwa walimu ambao wamekuwa na tabia ya kutowa kadi za ATM kwa wafanya biashara wanao kuwa wanawaidai fedha wajue kuwa walimu wanaofanya hivyo wanatia aibu kwenye jamii..
Afisa Elimu wa Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo alisema utaratibu huo wa kuwazadia zawadi walimu wastafu unawatia moyo walimu wengine kwani hapo nyuma wastafu walikuwa hawapewi mkono wa kwa heri .
Alisema chama cha walimu kinakwenda na wakati na ndio maana wameisha fungua benki ya walimu kwa ajiri ya kuwasaidia .
Nae Katibu wa CWT Mkoa wa Katavi Lucy Masegenya alisema utaratibu wa kuwapongeza na kuwapatia zawadi walimu wastafu ulianza kwaka jana na utaendelea kufanyika kila baada ya miezi sita kwa watakao kuwa wanastaafu kwenye kipindi hicho .
Alisema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na walimu katika Mkoa wa Katavi wamekuwa wakikatishwa tama na Afisa Elimu mmoja katika Manispaa hiyo ambae hakumtaja jina kuwa amekuwa akiwatolea lugha mbaya pamoja na kuwanyanyasa walimu pindi wanapokuwa wamefika osisini kwake kwa ajili ya kushughulikiwa matatizo yao .
Hivyo Chama cha Walimu CWT ngazi ya Mkoa na Wilaya wamepanga kwenda kumwona Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kumweleza jinsi anavyo wanyanyasa walimu na kama hata jirekebisha wako tayari kumkataa alisema Masegenya na kushangiliwa kwa nguvu na walimu waliokuwepo kwenye sherehe hizo .
Katibu wa CWT Wilaya ya Mpanda Wiliyson Masulwa alieleza kuwa chama hicho kimepanga kuanza kuwafundisha walimu ujasiliamali ili kuwapatia mbinu za kujiongezea kipato na ili waweze kutambua shughuli za ujasiliamali wakiwa bado wako kazini .
Alisema walimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni .
Kucheleweshewa malipo wastafu na mwanjiri kushindwa kuwarudisha makwao kwa wakati pindi wanapo kuwa wamestafu hari ambayo imekuwa ikiwaletea usumbufu mkubwa .
Pia wamekuwa hawashirikishwi kwenye kazi maalumu zennye malipo na badala yake wakekuwa wakitumiwa kwenye kazi maalumu ambazo hazina malipo .
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni majengo ya ofisi na madarasa yamejengwa bila kuzingatia mahitaji maalumu pamoja ukosefu wa vitavu vya kufundishia kwa ajiri ya walimu wasio ona
Mmoja wa walimu wastafu kutoka shule ya Msingi Igagala Moshi Rashid aliwataka wastafu wenzake na walimu wengine wajihadhari na wafanya biashara wa wanaopenda kuwatapeli walimu pindi wanapo stafu na wanapokuwa wamekalibia kustafu .
No comments:
Post a Comment