Home » » CWT MPANDA YATOA ZAWADI YA BATI KWA WALIMU WASTAAFU.

CWT MPANDA YATOA ZAWADI YA BATI KWA WALIMU WASTAAFU.


 Na  Walter  Mguluchuma .
    Katavi yetu Blog.
  Chama  cha  Walimu  Wilaya ya  Mpanda CWT kimewapatia  zawadi wastaafu wake walimu sita  waliostafu kuanzia  Januari  hadi  June  bati   120 zenye  thamani ya  shilingi  milioni  tatu ikiwa  ni  sehemu ya kutambua  mchango waliotoa  katika  utumishi wao wa  kazi ya elimu.

 Katika  zawadi  hizo za   mkono wa  kwa  heri kwa walimu  hao  sita wa kutoka   Manispaa ya  Mpanda  na   Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda  kila   mmoja  alipatiwa   bati  20.

  Zawadi  hizo walikabidhiwa  hapo juzi  katika sherehe za kuwapongeza walimu hao zilizofanyika  katika  ukumbi wa  Chekechea wa  Kanisa   Katoliki   Jimbo  la  Mpanda   ambapo   mgeni   rasmi  alikuwa ni  Katibu  Tawala wa  Mkoa wa  Katavi  Kamishina  Paulo  Chagonja aliyewakilishwa kwa niaba  yake  na  Afisa  Elimu wa  Mkoa  wa   Katavi  Erenesti   Hinju.

Katika hutuba  yake  aliyoitowa  Katibu   Tawala wa  Mkoa wa  Katavi kabla ya kukabidhi  zawadi  hizo  aliwataka walimu wanaokuwa  wanastafu   kuwacha  tabia yao ya maisha waliokuwa   nayo  sio wana  badilika  na kukimbia  familia zao pindi wapatapo  mafao yao .

 Alisema wastafu wengi  hasa walimu wamekuwa na tabia  ya kuchukua  mikopo kwenye taasisi za   Benki  binafsi na kwa wafanya biashara  mikopo yenye   liba kubwa  ambapo wakekuwa wakikopeshwa milioni 20 na wao wanalipa  milioni 40 kitu  ambacho kimewaathiri wastafu wengi  hivyo ni  vema wajiepushe na  liba za  namna  hiyo.

Imekuwa ni aibu kwa tabia   ilijengeka kwa walimu  ambao  wamekuwa  na  tabia ya  kutowa   kadi za   ATM  kwa  wafanya  biashara wanao kuwa wanawaidai fedha wajue kuwa walimu wanaofanya hivyo  wanatia  aibu  kwenye  jamii..

 Afisa  Elimu wa  Manispaa ya  Mpanda  Vicenti  Kayombo  alisema  utaratibu huo wa kuwazadia  zawadi walimu  wastafu  unawatia  moyo walimu  wengine  kwani  hapo  nyuma  wastafu walikuwa  hawapewi  mkono wa kwa  heri .

 Alisema  chama  cha  walimu  kinakwenda na wakati  na  ndio  maana  wameisha  fungua   benki ya  walimu  kwa ajiri ya kuwasaidia .

Nae   Katibu wa   CWT  Mkoa wa   Katavi  Lucy  Masegenya  alisema    utaratibu  wa kuwapongeza na kuwapatia zawadi walimu wastafu ulianza kwaka  jana na utaendelea kufanyika kila baada ya miezi sita kwa watakao kuwa wanastaafu kwenye kipindi  hicho .

 Alisema pamoja  na  jitihada  kubwa  zinazofanywa  na  walimu  katika   Mkoa wa Katavi  wamekuwa wakikatishwa  tama na Afisa   Elimu  mmoja  katika  Manispaa  hiyo  ambae  hakumtaja  jina  kuwa   amekuwa  akiwatolea  lugha  mbaya   pamoja  na kuwanyanyasa walimu pindi wanapokuwa wamefika osisini kwake kwa ajili ya kushughulikiwa  matatizo yao .

  Hivyo  Chama  cha   Walimu  CWT ngazi ya   Mkoa  na  Wilaya wamepanga kwenda kumwona   Mkurugenzi wa  Manispaa  hiyo  kumweleza  jinsi  anavyo wanyanyasa walimu  na  kama  hata  jirekebisha  wako tayari  kumkataa  alisema  Masegenya  na  kushangiliwa kwa  nguvu  na walimu waliokuwepo  kwenye  sherehe  hizo .

 Katibu wa  CWT  Wilaya ya  Mpanda   Wiliyson  Masulwa  alieleza kuwa   chama  hicho  kimepanga  kuanza    kuwafundisha  walimu  ujasiliamali   ili     kuwapatia  mbinu za kujiongezea kipato na ili  waweze  kutambua shughuli za ujasiliamali wakiwa bado wako kazini .

   Alisema  walimu  wanakabiliwa na  changamoto  mbalimbali  ambapo  alizitaja  baadhi ya  changamoto kuwa  ni .

 Kucheleweshewa malipo  wastafu  na  mwanjiri  kushindwa kuwarudisha  makwao  kwa wakati pindi wanapo  kuwa wamestafu hari  ambayo  imekuwa ikiwaletea  usumbufu  mkubwa .

 Pia  wamekuwa  hawashirikishwi  kwenye  kazi  maalumu  zennye  malipo  na  badala  yake wakekuwa wakitumiwa  kwenye  kazi  maalumu  ambazo  hazina  malipo .

Changamoto   nyingine  aliitaja  kuwa   ni  majengo ya  ofisi na  madarasa  yamejengwa  bila kuzingatia  mahitaji  maalumu  pamoja  ukosefu wa  vitavu vya  kufundishia  kwa  ajiri ya walimu wasio  ona
  Mmoja wa  walimu wastafu kutoka  shule ya  Msingi  Igagala   Moshi   Rashid  aliwataka wastafu wenzake  na walimu  wengine wajihadhari  na wafanya  biashara wa  wanaopenda kuwatapeli walimu  pindi wanapo stafu na wanapokuwa wamekalibia kustafu .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa