Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu Blog
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Genelali Mstafu Raphael Muhuga ametowa agizo la kuwataka watu waliovamia na kuishi kwenye hifadhi za Mistu,Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye vyanzo vya maji waondoke kwa hiyari yao vinginevyo wataondolewa kwa nguvu .
Muhuga alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari ofisini kwake wakati akitowa taarifa mbalimbali za maendeleo ya Mkoa wa Katavi .
Alisema Mkoa wa Katavi upo hatarini kuwa jangwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kutoka na uharibifu mkubwa unaofanywa wa kuharibu mazingira hasa ukatwaji wa miti ovyo na watu kuishi katika maeneo yasiyositahili kuishi .
Alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa michache ambayo inahuhakika wa kupata mvua hivyo Mkoa kama hautakuwa makini upo uwezekano wa kupotea kwa mvua hizo .
Alisema ameisha towa agizo kwa wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Katavi ya kuhakikisha watu wote waliovamia na kuishi kwenye maeneo ya Hifadhi za mistu na kwenye vyanzo vya maji waondoke kwa hiari yao kwa kipinndi cha mwezi mmoja kuanzia sasa baada ya mwezi mmoja wale wote watakao kaidi wataondolewa kwa nguvu .
Alieleza kuanzia sasa ni marufu katika Mkoa wa Katavi mtu au watu kufanya shughuli zozote ambazo zinaharibu mazingira .
Alitaja baadhi ya uharibifu unaofanywa katika Mkoa huo ni ukataji miti ovyo , uchomaji wa mkaa mifugo kuchungiwa ndani ya hifadhi ya Katavi ,kwenye mistu na watu kuishi katika maeneo yasiyo sitahili kuishi ukatavi wa magogo na miti ovyo.
Na endapo wataendelea watu kuachiwa waendelee wataleta uharibifu mkubwa sana wa mistu iliyopo kwa sasa kwani Mkoa huu ni mkoa pekee wenye eneo kubwa la mistu yenye uoto wa asili .
Rc Muhuga alisema karibu maeneo yote ya Mkoa wa Katavi kwa Katavi kunauharibifu wa mazingira ya ukatwaji miti ovyo hasa kwenye maeneo ya barabara ya Mpanda Tabora,Mpanda Kigoma Mpanda Karema na Mpanda Mpimbwe,
Na uharibufu unaofanywa sasa unafanyika kwa ndani ya mistu kuliko ilivyo kwa pembeni ya barabara alisema Meja Genelali Muhuga .
No comments:
Post a Comment