Na Walter Mguluchuma Na Arine Temu .
Katavi .
Wamiliki na madreva wa Aice wanaofanya safari zao za kusafirisha abiria katika stendi kuu ya Mpanda Mkoani Katavi wamegoma kufanya safari zao hapo jana kwa kile wanachodai kuchoshwa na fedha wanazotozwa na Askari wa usalama barabarani zinazoitwa safari Book kila waondokapo, na wanapokuwa njiani na kwenye kituo wanachoishia safari .
Wamiliki na madreva waliogoma ni wale wanaofanya safari zao kwenda Ugala , Inyonga Wilaya ya Mlele , Ikola na Vikonge Wilaya ya Tanganyika pamoja na Kakese Mwamkulu Manispaa ya Mpanda .
Baadhi ya wamiliki hao waliwaambia wandishi wa Habari jana kwenye stendi kuu ya Mpanda kuwa hawako tayari kufanya safari zao mpaka hapo askari wa usala barabarani watakapokuwa wamewaondolea malipo yasiyotambulika wanayoyaita Book safari ambapo wamekuwa wakizwa kwenye kituo cha ofisi ya usama barabarani iliyoko katika Stendi hiyo .
Mmoja wa wa wamiliki wa Aice inayofanya safari zake toka Mpanda kwenda Ikola Daudi Kiula alisema wamekuwa wakitoozwa kiasi cha Tsh 5,000 kila wanapotoka kwenye stendi kuu na wanapofika kwenye kituo cha kukaguliwa wanatozwa tena Tsh 5,000 na wanapofika kwenye kituo cha mwisho wamekuwa wakitozwa tena Tsh 5,000.
Hivyo kwa safari moja wamekuwa wakitozwa Tsh 15,000 kwa safari ya kwenda na kurudi wamekuwa wakitozwa kiasi cha shilingi elfu thelasini kwa kila Aice moja .
Abeli Kambaulaya anae fanya safari zake Mpanda .inyonga alisema kuwa fedha hizo wanazotozwa zimekuwa ni kero kubwa sana ndio maana tumeamua tusitishe safari zetu mpaka hapo tutakapo elezwa kama kweli malipo hayo yapo kwa mujibu wa sheria .
Kwa upande John Mwananyama ambae ni mkatishaji wa tiketi ya Aice inayofanya safari zake kwenda Ugala Wilayani Mlele aliwaambia wandishi wa habari wamekuwa wakipewa fomu na askari wa usalama barabarani inayoitwa Book safari ambayo huwa wanajaziwa kila wanapolipia wanapo kuwa wanaondoka na wasipofanya hivyo huwa wanatozwa faini ya Tsh 30,000.
Fomu hiyo wanayojaziwa kila wanapokuwa kuwa wamelipia haina hata nembo yoyote ile ya Serikali embu tazameni hata nyie Wandishi wa Habari alisema huku akiwa anaonyesha fomu hiyo ya boo safari .
Mmoja wa abiria Salome John alisema yeye ameshuka leo yaani jana na treni akiwa anatoka Mwanza kwa kutegemea angesafiri kwenda kwake Ikola lakini kutokana na mgomo huo atalazimika kulala kwenye stendi kwani hana fedha za kulala gesti kwani hana ndugu hapa mjini Mpanda .
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi hakuweza kupatikana ili aweze kuelezea ufumbuzi wa mgomo huo.
No comments:
Post a Comment