Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Rais wa Muungano wa Klabu za Wandishi wa Habari Tanzani UTPC Deo Nsokolo amewataka Wandishi wa Habari hapa Nchini wajiunge na mfuko wa Bima ya Afya ili waweze kunufaika na mfuko huo pindi wanapokuwa wameugua .
Nsokolo alitowa kauli hiyo hapo jana alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari wa Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kwenye ofisi za Chama hicho iliyopo katika Mtaa wa Madukani Mjini Mpanda wakati wa ziara yake .
Alisema umefika wakati R kwa kila Mwandishi wa Habari ambao ni wanachama wa vyama vya wandishi wa Habari vya Mikoa na wale ambao sio wanachama wawekewe utaratibu wa kujiunga na Bima ya Afya kwani inamanufaa sana pindi mtu anapokuwa ameugua .
Alifafanua kuwa wandishi wengi wa Habari kipato chao ni kidogo sana hivyo watakapo kuwa wamejiunga na Bima ya Afya watapata manufaa ya kutibiwa kwa gharama nafuu wao na watemezi wao .
Rais huyo wa UTPC alisema ni vema vyama vya wandishi wa Habari vikawa na utaratibu wanapokuwa wanawapokea wanachama wapi wanaokuwa wanaomba kujiunga na vyama vyao vya wandishi wa Habari wakawekewa utara wa kuiunga na Bima ya Afya .
Aidha aliwataka wandishi wajihadhari wanapofanya kazi wahakikishe wanafanya kazi katika misingi ambayo itawafanya wawe salama .
Alisema wandishi wa Habari hawana nia mbaya kwenye jamii ila watu wangine wamekuwa wamekuwa wakiwafikilia vibaya na kutishia usama wao .
MWISHO
No comments:
Post a Comment