Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wizara ya Maliasili na Utalii imewahimiza wanahabari kujiunga na mafunzo ya kijeshi yanayotolwa na shirika la Hifadhi Taifa TANAPA ili waweze kuzielewa changamoto zake badala ya kuandika na kutangaza habari zake tuu.
Ushawishi huo ulitolewa na Katibu mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenarali Gaudensi Milanzi wakati akifunga mafunzo ya Askari wa Tanapa na uhifadhi wa Ngorongoro .
Alisema Tanapa ipo katika kubadili mfumo wa utendaji wa kazi kutoka ule wa kiraia kuwa jeshi Usu Paramlltary System ili kukabiliana na tatizo sugu la ujangili wa wanyama mistu na rasilimali nyngine za Nchi .
Badala ya wandishi wa habari kuja kila siku huku na kuandika na kutangaza habari zetu sasa nyinyi tunawaalika mjiunge nasi katika mafunzo ya kijeshi hii itasaidia sana kutambua changamoto zetu pia kujenga afya ya akili na mwili kwa kufanya mazoezi .
Akizungumza alisema maombi ya Tanapa kutaka kubadilishwa na kuendeshwa kwa sheria za Kijeshi ni yamsingi katika kipindi hiki ambacho Tanzania inakabiliwa na tatizo sugu la ujangili wa wanyama pori .
Ufungaji wa mafunzo hayo ulifanyika juzi katika kambi ya Mlele Mkoa wa Katavi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo Mameneja 10 na Askari 58 kutoka Tanapa na uhifadhi wa Ngorongoro walihitimi mafunzo hayo ya mwezi mmoja .
Naamini pasipo shaka mafunzo yatawasaidia kuimarisha nidhamu kipindi hiki tunachojiandaa kuingia katika mfumo tarajiwa wa kiutendaji wa jeshi Usu .
Kwa sasa uhifadhi unakabiliwa na changamoto kubwa ya ujangili hususani wa Tembo na Faru kuporomoka kwa maadili kwa baadhi ya askari wa Tanapa na uingizwaji wa mifugo Hifadhini alisema Meja Jenerali Milanzi .
Alisema sheria ya uanzishwaji wa jeshi Usu ilichelewa kutekelezwa ambapo ikiendelea kucheleweshwa itasababisha kuchelewa kupatikana kwa vitendea kazi vya kisasa .
Hata hivyo aliwakaka Askari hao pamoja na Menejimenti kufanya maandalizi ya kutosha kwa misingi ya kuwa na sheria itayopitishwa baadhi ya mabadilio na uendeshaji kwa utaratibu wa kama majeshi mengine
Awali akiwasilisha maombi hayo Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi alisema shirika hilo baada ya kutafakari kwa kina kwa kutumia watalamu wake wa ndani walibaini umuhimu wa askari wao kutumia sheria za kijeshi kutokana na changamoto ya sasa katika maswala ya uhifadhi .
Nae Meneja wa mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi Joseph Mwang-ombe alisema kambi hiyo ya Mlele inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo uwanja wa ndege kutokalabatiwa kwa wakati , uchakavu wa majengo na miundo mbinu ya maji pamoja na mawasiliano ya simu .
Wakiongea na gazeti hili wandishi wa Habari Alslaji Mvungi w ITV Ar usha , Joshua Joel Itv Rukwa Adolfu Mbata Tbc Katavi ,Bibada Erenest Azamu Katavi na Pety Siame Habari Leo Rukwa walisema kuwa wao wako tayari kujiunga na mafunzo hayo pindi watakapo kuwa wamehitajika kufanya mafunzo hayo.
0 comments:
Post a Comment