Friday, July 8, 2016

WAFUGAJI KATAVI KWENDA RWANDA KUJIFUNZA UFUGAJI BORA


   Na   Walter   Mguluchuma
       Katavi
    Chama  cha  Wafugaji  CCWT   Mkoa  wa  Katavi  kinatarajia  kuwapeleka  Nchi ya  Rwanda  baadhi ya  wafugaji wa  mifugo  ya  Ng-ombe  kwenda   kujifunza   elimu ya  ufugaji  bora wa  kisasa.
Hayo  yalisemwa  hapo juzi   na   Mwenyekiti  wa   Chama   cha  Wafugaji  cha   Mkoa  wa Katavi  Mussa  Kabushi kwenye  kikao  cha  wafugaji wa  mifugo  kilichowashirikisha  wafugaji wa   kutoka  Halmashauri  zote   tano za  Mkoa  wa   Katavi pamoja   na wenyeviti wa  Halmashauri   na   Madiwani  kutoka   katika   Halmashauri  hizo  kilichofanyika   katika  ukumbi wa  Galden  Mjini  Mpanda.
  Alisema  tatizo   linalowakabili wafugaji wengi  hapa  Nchini  ni  ukosefu wa  elimu  bora ya ufugaji wa kisasa kwa  kutambua hilo  ndio  maana   chama  cha  wafugaji  cha  Mkoa wa   Katavi kimeamua kuandaa  utaratibu wa  kuwapeleka  baadhi ya  wafugaji  Nchini  Rwanda  ili wakapate  ili ya  ufugaji bora wa  kisasa.
 Alieleza   kiliokikubwa  kwa  sasa  kwa  wafugaji wa  Mkoa wa  Katavi ni kutotengewa  eneo la kufugia  mifugo hari  ambayo  imekuwa  ikiwafanya baadhi ya wafugaji kufugia  kwenye  maeneo  yasiyo  sitahili  hivyo wanaiomba  Serikali ya  Mkoa  wa  Katavi  kuharakisha kuwapatia  maeneo ya kuchungia  mifugo yao .
 Aliwaka  wafugaji wajitambue kuwa  wao ni   wawekezaji wa  ndani  na  pia ni  matajiri  wakubwa  kutokana  na  mifugo  walio  kuwa  inayo kwani  kipata  wanachopata  ni  kikubwa  hata  kuzidi  wanachopata  baadhi ya  watumishi wa   Serikali .
Meya  wa   Manispaa ya  Mpanda  Willy  Mbogo  aliviomba   vijiji  vyenye  maeneo  ya   ardhi  kutenga  maeneo kwa   ajiri ya  wafugaji  ili  kuweza  kuondoa  migogoro  baina  ya  wakulima  na  wafugaji .
 Aliwataka  wafugaji  kujenga  tabia  ya kuishi kwa  kutii  sheria  na kutunza  mazingira  na  wafuge  kisasa  wasiwe  wachungaji   bali  wawe  wafugaji .
Mwenyekiti wa  Halmashauri ya  Nsimbo  Raphael  Kalinga   alisema  kumekuwepo  na   changamoto kubwa ya  wafugaji  katika   Mkoa  wa   Katavi  ya  kuhamishia  mifugo  kutoka  sehemu  nyingine   bila  kufuata  sheria   Namba  tano  ya   ardhi   hari   ambayo   inafanya  kutokea  kwa  migogoro   baina  ya  Serikali  na  wafugaji .
 Pia  aliwataka  wafugaji  waache  tabia  ya  kusafirisha  mifugo  kwenye  maeneo  yasiyo   sitahili kwani kufanya  hivyo ni  kosa  na  matokeo  yake  wanapokuwa  wanakamatwa wanaona  kuwa ni kama  wanaonewa .
Nae   Mfugaji   Masanja   Ndekeja  wa  Kijiji  cha   Chamalendi   Mpimbwe  W ilaya ya    Mlele  alidai  kuwa  wafugaji wamekuwa  wakinyanyaswa  na  watendaji wa  vijiji na  Kata kwa kutozwa  faini za kuanzia  tsh  300,000  hata   kama  mifugo  yao  haija   haribu  mazao ya  wakulima   hivyo  wao  wanafanywa  kama ATM  ya  kutolea   fedha   Banki

No comments:

Post a Comment