Na Walter Mguluchuma
Katavi
Chama cha Wafugaji CCWT Mkoa wa Katavi kinatarajia kuwapeleka Nchi ya Rwanda baadhi ya wafugaji wa mifugo ya Ng-ombe kwenda kujifunza elimu ya ufugaji bora wa kisasa.
Hayo yalisemwa hapo juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji cha Mkoa wa Katavi Mussa Kabushi kwenye kikao cha wafugaji wa mifugo kilichowashirikisha wafugaji wa kutoka Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi pamoja na wenyeviti wa Halmashauri na Madiwani kutoka katika Halmashauri hizo kilichofanyika katika ukumbi wa Galden Mjini Mpanda.
Alisema tatizo linalowakabili wafugaji wengi hapa Nchini ni ukosefu wa elimu bora ya ufugaji wa kisasa kwa kutambua hilo ndio maana chama cha wafugaji cha Mkoa wa Katavi kimeamua kuandaa utaratibu wa kuwapeleka baadhi ya wafugaji Nchini Rwanda ili wakapate ili ya ufugaji bora wa kisasa.
Alieleza kiliokikubwa kwa sasa kwa wafugaji wa Mkoa wa Katavi ni kutotengewa eneo la kufugia mifugo hari ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya wafugaji kufugia kwenye maeneo yasiyo sitahili hivyo wanaiomba Serikali ya Mkoa wa Katavi kuharakisha kuwapatia maeneo ya kuchungia mifugo yao .
Aliwaka wafugaji wajitambue kuwa wao ni wawekezaji wa ndani na pia ni matajiri wakubwa kutokana na mifugo walio kuwa inayo kwani kipata wanachopata ni kikubwa hata kuzidi wanachopata baadhi ya watumishi wa Serikali .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo aliviomba vijiji vyenye maeneo ya ardhi kutenga maeneo kwa ajiri ya wafugaji ili kuweza kuondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji .
Aliwataka wafugaji kujenga tabia ya kuishi kwa kutii sheria na kutunza mazingira na wafuge kisasa wasiwe wachungaji bali wawe wafugaji .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Raphael Kalinga alisema kumekuwepo na changamoto kubwa ya wafugaji katika Mkoa wa Katavi ya kuhamishia mifugo kutoka sehemu nyingine bila kufuata sheria Namba tano ya ardhi hari ambayo inafanya kutokea kwa migogoro baina ya Serikali na wafugaji .
Pia aliwataka wafugaji waache tabia ya kusafirisha mifugo kwenye maeneo yasiyo sitahili kwani kufanya hivyo ni kosa na matokeo yake wanapokuwa wanakamatwa wanaona kuwa ni kama wanaonewa .
Nae Mfugaji Masanja Ndekeja wa Kijiji cha Chamalendi Mpimbwe W ilaya ya Mlele alidai kuwa wafugaji wamekuwa wakinyanyaswa na watendaji wa vijiji na Kata kwa kutozwa faini za kuanzia tsh 300,000 hata kama mifugo yao haija haribu mazao ya wakulima hivyo wao wanafanywa kama ATM ya kutolea fedha Banki
0 comments:
Post a Comment