Na Walter Mguluchuma
Katavi
Akina Mama wajawazito wanaokwenda kujifungulia kwenye Zahanati ya Kata ya Simwesa Wilaya mpya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wanalazimika kujifungulia kwenye chumba kimoja kinachokuwa wamelazwa wagojwa wengine wakiwemo wakiume kutokana na Zahanati hiyo kukabiliwa na uhaba wa vyumba vya kulaza wagonjwa .
Hayo yalielezwa juzi na Diwani wa Kata ya Simbwesa Duus Masunga wakati wa kikao cha nne cha kawaida cha Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mpanda kwa sasa ni Wilaya mpya ya Tanganyika kilichofanyika katika ukumbi wa idara na kilochoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hamad Mapengo .
Diwani Masunga alilieleza Baraza hilo la Madiwani kuwa wakina Mama wajawazito wanaoishi kwenye Kata yake ya Simbesa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kujifungulia kwene chumba kimoja ambacho kinatumiwa pia kulaza wagonjwa wengine wakiwemo wagojwa wa kiume .
Alisema Kata hiyo ya Simbesa ilianzishwa mwaka 1973 kwa sasa ina jumla ya Kaya zipatazo 31,250,000 na vijijiji vitatu inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyumba vya kulazia wagonjwa kwa kipindi kirefu sasa huku zahanati hiyo ikiwa na chumba kimoja tuu kinachotumika kwa ajiri ya kulazia wagonjwa wa jinsia zote na pia kinatumika kwa ajiri ya kutolea matibabu ya wagonjwa waaina zote .
Aliendelea kulieleza baraza hilo kuwa wakina mama wajawazito wanaokwenda kujifungulia kwenye Zahanati hiyo nyakati za usiku ndio wamekuwa wakipata shida kubwa pindi wanapokuta chumba hicho kinapokuwa na wagonjwa wengine wakipatiwa huduma .
Aliliomba Halmashauri hiyo kufanya haraka kujenga vyumba vingine vya kutolea huduma na kulaza
wagonjwa kwenye zahanati hiyo ili kuokoa uhai wa mama na mtoto kwa wakazi wa Kata hiyo.
Alisema zahanati hiyo inatowa huduma kwa wakazi wa Vjiji vya Kungwa, Simwesa na Kabage na baadhi ya wananchi wanalazimika kutembea umbali wa kiliometa 30 hadi kufika kwenye zahanati hiyo.
Diwani wa Kata Kasangantongwe Tarafa ya Karema Osca Sangu alisema kuwa matizo ya Kata ya Simwesa yanataka kulingana na yale ya Kata yake .
Alisema kwenye Kata yaKE hakuna huduma zozote zinazotolewa hata za mama na mtoto kutokana na zahanati iliyojengwa kwenye Kata hiyo kutokuwa na mganga hata mmoja na pia haina hata choo.
Chakushangaza zahanati hiyo imepelekewa dawa ambazo zimekaa tuu na upo uwezekano mkubwa wa dawa zilizopelekwa hapo zikaisha muda wake ni vema dawa hizo zikachukuliwa na kupelekwa kwenye maeneo mengine alisema Diwani huyo kwa masikitiko makubwa .
Mratibu wa Huduma za wagonjwa majumbani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda sasa Tanganyika Medadi Adrea ambae alimwakilisha Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo alieleza Baraza hilo la madiwani kuwa wameshindwa kupeleka mganga kwenye zahanati ya Kasagantongwe kwa kuwa hakuna nyumba ya kuishi mganga wala muhuguzi .
Alimwombo Diwani wa Kata hiyo kama atakuwa yuko tayari kumpangisha chumba kwenye nyumba yake mganga watakae mpagia kwenda kufanya kazi hapo wao wako tayari kupeka mganga kwenye Zahanati hiyo .
No comments:
Post a Comment