Na Walter Mguluchuma
Katavi
Meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Mpanda Mkoa wa Katavi Willy Mbogo amewashauri wafugaji wafundishwe mafunzo ya elimu ya ujasiliamali ili waachane na tabia ya kutegemea mifugo peke yake .
Mbogo alitowa ushauri huo hapo juzi wakati alipokuwa akifungua kikao cha wafugaji wa kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa Galden Mjini hapa .
Alisema wafugaji wengi wamekuwa wamekuwa wakitegemea kuendesha maisha yao kwa kutegemea mifugo yao hivyo ni vizuri wakaanza kupewa mafunzo ya ujasiliamali ili waweze kuachana na tabia ya kutegemea mifugo peke yake .
Pia alisema ni vizuri wafugaji wafundishwe kupunguza mifugo yao ili waweze kuendeleza shughuli nyingine za kibiashara kama vile ujenzi wa nyumba za kulala wageni.
Aliwaeleza Mkoa wa Katavi upo kwenye mchakato wa kuanzisha Banki ya Wananchi wa Mkoa wa Katavi hivyo wafugaji wakubali kujiunga na banki hiyo pindi itakapoanza kwa kunuua hisa .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Raphael Kalinga alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto ya wafugaji kuhamia kiholela kutoka katika mikoa ya Kanda ya ziwa
Nae Mwenyekiti wa chama cha Wafugaji cha Mkoa wa Katavi CCWT Mussa Kabusha alieleza kuwa tatizo kubwa linalowakabili w afugaji wa Mkoa wa Katavi ni kukosekana kwa eneo la wafugaji ingawa Serikali ya Mkoa wa Katavi imeisha waahidi kutenga eneo kwa ajiri ya wafugaji .
Alisema chama cha wafugaji cha Mkoa wa Katavi kilianzishwa mwaka 2014 na kilipoanzishwa kulikuwa na m igogoro na Serikali lakini migogoro hiyo kwa sasa haipo hasa baada ya kuondolewa viongozi wa awali wa chama cha wafugaji .
Mjumbe wa Bodi ya Wafugaji Tanzania Beda Katani alieleza kuwa baadhi ya watendaji ndani ya serikali ndio wamekuwa wakichangia migogoro ya wafugaji na wakulima .
Katika swala la wafugaji Serikali haina cha kujitetea kwa wafugaji kwani haijawatengea maeneo ya kufugia hari ambayo imekuwa ikichangia migogoro ya mara kwa mara baina wafugaji na Tanapa Maliasili na wakulima alisema Katani.
Kwa upande wake mfugaji Elizabethi Kabija aliliomba Serikali ya Mkoa wa huu kuwatengea maeneo wafugaji iliwaepukane na migogoro baina yao na wakulima .
Cherehani Maombi alilamika kuwa kwenye vijiji mbalimbali kulikuwa maeneo ambayo yalikuwa yametengwa kwa ajiri ya wafugaji lakini viongozi wa vijiji wamebadilsha maeneo hayo na kuwa makazi ya watu .
Aliendelea kusema hivyo maeneo yote yalikuwa yametengwa kwa ajiri ya wafugaji wanaomba maeneo hayo war udishiwe kwani hawana maeneo ya kufugia mifugo yao .
No comments:
Post a Comment