Home » » TUKIO RASMI KATIKA PICHA: BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VIFAA KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI

TUKIO RASMI KATIKA PICHA: BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VIFAA KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Meneja wa nmb Happtnes Pima akikabidhi computer nne printe moja na laptop moja kwa mkuu wa mkoa ili aweze kukabidhi kwa wanahabari wa mkoa wa katavi mkuu wa mkoa alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
 RC katavi Raphael Muhuga akimkabidhi Mwenyekiti wa katavi press klab Walter Mguluchuma naye akabidhi kwa makamu mwenyekiti wa klabu. ​
 Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga iakikabidhi vifaa vilivyotolewa na benki ya NMB Tawi la mpanda hafla hiyo ilifanyika ofis ya klab ya waandishi mtaa wa madukani mjini mpanda.​
 Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga iakikabidhi vifaa vilivyotolewa na benki ya NMB Tawi la mpanda hafla hiyo ilifanyika ofis ya klab ya waandishi mtaa wa madukani mjini mpanda.​
Picha ya pamoja ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa katavi Raphael Muhuga na wafadhili waliotoa vifaa vya kazi kwa waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa klabu ya waandishi wa habari ​ 

PICHA ZOTE NA KIBADA ERNEST KIBADA MWANACHAMA WA KATAVI PRESS CLUB

NA   Mwandishi  wetu  KATAVI
Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi imepokea msaada wa vifaa  kwa ajili ya kusaidia kurahisha shuhuli za habari kwa waandishi wa habari wa mkoa huo  vifaa hivyo ni computer za  mezani Desktop nne,Printer moja ya rangi na Computer moja ya mkononi laptop kutoka benki ya NMB    vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Katavi Walter Mguluchuma  akipokea msaada huo ameshukuru kwa msaada uliotolewa na benki ya NMBakaomba wadau wengine waendelea kusaidia.
Amesema msaada huo umekuja  kwa wakati mwafaka na utasaidia kwa njia mmoja au nyingine kupunguza changamoto ya vitendea kazi inayokabili klabu ambayo bado ni  changa hivyo Benki ya NMB imesaidia sana kutoa msaada huo ambao utarahisha utendaji kazi.
Akaongeza kuwa klabu ilipokea msaada mwingine wa vifaa kutoka kwa mlezi wa klabu nchini yaani Muungano wa Klab za waandishi wa Habari nchini UTPC  na vifaa hivyo ndiyo vinavyotumika katika kurahisha kazi ya habari kwa wanahabari wa katavi, miongoni mwa vifaa hivyo ni camera ya picha za mnato,na picha za video, computer za mezani  nne,laptop printer,scanner,projector pamoja na TV Screen.
Mwenyekiti  ameomba benki hiyo isichoke kuendelea kusaidia pale watakapoweza  kwa kuwa bado kunauhitaji  ni mkubwa wa vitendea kazi kama camera za picha za video ,taprecorder pamoja na msaada mingine ya hali na mali,  akaomba na wengine kujitokeza kusaidia pale watakapoweza na milango iko wazi kwa wadau kusaidia.
Mkuu wa Mkoa wa KATAVI Meja Jenerali  Mstaafu Raphael Muhuga  ametoa rai kwa  wadau wa Habari taasisi mbalimbali zilizoko mkoani humo wafanyabiashara  wasiachie benki ya NMB pekee klabu ya waandishi wa Habari vifaa vya akazi kama kamera hazitoshi tena za aina mbalimbali wajitokeze kusaidia.
Amesema wasiachie benki ya NMB  pekee yao kutoa msaada anaamini uwezo upo wajitokeze kwa kuwa klabu bado ni changa hivyo wanahitaji msaada bado vinahitajika msaada zaidi wajitokeze kusaidia  vyombo vya habari mkoani humo ili viweze kufanyakazi kwa uhakika zaidi na kupatikana kwa vifaa kutasaidia kutawawezesha kufanya kazi kwa uhakika.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema  yeye kama mkuu wa mkoa anathamini mchango mkubwa  unaotolewa na vyombo vya Habari kuwa vinamchango mkubwa  katika kuleta maenndeleo makubwa kwa mkoa na Taifa.
Amesema ipo nafasi kubwa kwa kila mdau katika mkoa kusaidia kwa hali na mali ili kuimarisha klabu ya waandishi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufasaha Zaidi, kwa kuwa vyombo vya habari ni mmoja kati ya mihimili mine hata kama ungefanya vizuri bila kutangaza mambo yako ni bure.
Hakuna atakaye fahamu kama unafanya mambo mazuri,akatoa mfano mkoa wa katavi umefanya vizuri katika elimu kwa kushika nafasi ya Kwanza kitaifa lakini hakuna aliyefahamu bila kutumia vyombo vya habari,pia akatoa mfano alipokuwa anafanyaziara kujitambulisha alitumia vyombo vya habari taarifa nyingi zitawafikia kwa haraka na bila kupotoshwa.
Pamoja na kupongeza Benki ya  NMB kuthamini Mchango wa vyombo vya habari pia  yeye kama mkuu wa mkoa anaelewa umuhimu wa vyombo vya Habari kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuwafika wananchi zaidi ya robo tatu katika mkoa ikitokea taarifa yeyote ya msingi unayotaka ifike,  ukisema ufanye ziara huwezi kupita vijiji vyote na huwezi  kufika kila  mtu lakini kupitia vyombo vya habari taarifa nyingi zitawafikia wananchi haraka  na zitafika bila kupotoshwa.
Katika ziara zake alizofanya  mkoani wakati anajitambulisha alipata fursa ya kutembelea maeneo mengi ikiwa ni pamoja na  makazi ya katumba na mishamo alitoa ujumbe kule  na ule ujumbe uliwafikia siyo wale tu waliohudhuria bali pia wananchi wengine kwa sababu taarifa ile hawahusu wale tu pekee yao .suala la kuishi kama watanzania haliwahusu wale tu pekee yake  ni pamoja na   raia wengine wanaishi hapa mikoani  kujua sasa tunao raia wengine wapya 162,000 wa mkioa miwili ya katavi na tabora watambue kuwa tuaingiliana katika maeneo mbalimbali  ya maisha ya kijamii mitaani.  hivyo vyombo vy ahabari vina mchangokubwa sana.
 Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB  Mkoa wa Katavi Happtnes Pima  ameeleza lengo kuu la kuwatoa vifaa hivyo ambavyo ambavyo ni computer desk top nne, printer moja na laptop moja vyote  vikiwa na   thamani ya zaidi ya shilingi  milioni tano za kitanzania lengo kubwa  ni kuwa  benki ya nmb  ni ya   wananchi.
 Faida wanayoipata wanachangia na wananchi hivyo wanathamini mchango wa waandishi wa Habari kwa sababu wanawafikia wananchi wanafanya kazi kwa wananchi naNMB nibenki yao ,
Pimma akaongeza katika moja ya vipaumbele vyao kwa mwaka huu  ni kutoa  huduma  kwa wateja ,na waandishi wa Habari nao wanatoa huduma  kwa wananchi hivyo huo ni utamaduni wa benki ya NMB.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa