Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja wa nmb Happtnes Pima akikabidhi computer nne printe moja na
laptop moja kwa mkuu wa mkoa ili aweze kukabidhi kwa wanahabari wa mkoa
wa katavi mkuu wa mkoa alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
RC katavi Raphael Muhuga akimkabidhi Mwenyekiti wa katavi press klab
Walter Mguluchuma naye akabidhi kwa makamu mwenyekiti wa klabu.
Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga iakikabidhi
vifaa vilivyotolewa na benki ya NMB Tawi la mpanda hafla hiyo ilifanyika
ofis ya klab ya waandishi mtaa wa madukani mjini mpanda.
Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga iakikabidhi
vifaa vilivyotolewa na benki ya NMB Tawi la mpanda hafla hiyo ilifanyika
ofis ya klab ya waandishi mtaa wa madukani mjini mpanda.
Picha ya pamoja ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari na mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa katavi Raphael Muhuga na wafadhili waliotoa vifaa
vya kazi kwa waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa klabu ya
waandishi wa habari
PICHA ZOTE NA KIBADA ERNEST KIBADA MWANACHAMA WA KATAVI PRESS CLUB
NA Mwandishi wetu KATAVI
Klabu
ya waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi imepokea msaada wa vifaa kwa
ajili ya kusaidia kurahisha shuhuli za habari kwa waandishi wa habari wa
mkoa huo vifaa hivyo ni computer za mezani Desktop nne,Printer moja
ya rangi na Computer moja ya mkononi laptop kutoka benki ya NMB vyote
vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Katavi Walter Mguluchuma
akipokea msaada huo ameshukuru kwa msaada uliotolewa na benki ya
NMBakaomba wadau wengine waendelea kusaidia.
Amesema
msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka na utasaidia kwa njia mmoja au
nyingine kupunguza changamoto ya vitendea kazi inayokabili klabu ambayo
bado ni changa hivyo Benki ya NMB imesaidia sana kutoa msaada huo ambao
utarahisha utendaji kazi.
Akaongeza
kuwa klabu ilipokea msaada mwingine wa vifaa kutoka kwa mlezi wa klabu
nchini yaani Muungano wa Klab za waandishi wa Habari nchini UTPC na
vifaa hivyo ndiyo vinavyotumika katika kurahisha kazi ya habari kwa
wanahabari wa katavi, miongoni mwa vifaa hivyo ni camera ya picha za
mnato,na picha za video, computer za mezani nne,laptop
printer,scanner,projector pamoja na TV Screen.
Mwenyekiti
ameomba benki hiyo isichoke kuendelea kusaidia pale watakapoweza kwa
kuwa bado kunauhitaji ni mkubwa wa vitendea kazi kama camera za picha
za video ,taprecorder pamoja na msaada mingine ya hali na mali, akaomba
na wengine kujitokeza kusaidia pale watakapoweza na milango iko wazi
kwa wadau kusaidia.
Mkuu
wa Mkoa wa KATAVI Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ametoa rai kwa
wadau wa Habari taasisi mbalimbali zilizoko mkoani humo
wafanyabiashara wasiachie benki ya NMB pekee klabu ya waandishi wa
Habari vifaa vya akazi kama kamera hazitoshi tena za aina mbalimbali
wajitokeze kusaidia.
Amesema
wasiachie benki ya NMB pekee yao kutoa msaada anaamini uwezo upo
wajitokeze kwa kuwa klabu bado ni changa hivyo wanahitaji msaada bado
vinahitajika msaada zaidi wajitokeze kusaidia vyombo vya habari mkoani
humo ili viweze kufanyakazi kwa uhakika zaidi na kupatikana kwa vifaa
kutasaidia kutawawezesha kufanya kazi kwa uhakika.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema yeye kama mkuu wa mkoa anathamini mchango mkubwa
unaotolewa na vyombo vya Habari kuwa vinamchango mkubwa katika kuleta
maenndeleo makubwa kwa mkoa na Taifa.
Amesema
ipo nafasi kubwa kwa kila mdau katika mkoa kusaidia kwa hali na mali
ili kuimarisha klabu ya waandishi ili waweze kufanya kazi zao kwa
ufasaha Zaidi, kwa kuwa vyombo vya habari ni mmoja kati ya mihimili mine
hata kama ungefanya vizuri bila kutangaza mambo yako ni bure.
Hakuna
atakaye fahamu kama unafanya mambo mazuri,akatoa mfano mkoa wa katavi
umefanya vizuri katika elimu kwa kushika nafasi ya Kwanza kitaifa lakini
hakuna aliyefahamu bila kutumia vyombo vya habari,pia akatoa mfano
alipokuwa anafanyaziara kujitambulisha alitumia vyombo vya habari
taarifa nyingi zitawafikia kwa haraka na bila kupotoshwa.
Pamoja
na kupongeza Benki ya NMB kuthamini Mchango wa vyombo vya habari pia
yeye kama mkuu wa mkoa anaelewa umuhimu wa vyombo vya Habari kwa sababu
ndiyo njia pekee ya kuwafika wananchi zaidi ya robo tatu katika mkoa
ikitokea taarifa yeyote ya msingi unayotaka ifike, ukisema ufanye ziara
huwezi kupita vijiji vyote na huwezi kufika kila mtu lakini kupitia
vyombo vya habari taarifa nyingi zitawafikia wananchi haraka na
zitafika bila kupotoshwa.
Katika
ziara zake alizofanya mkoani wakati anajitambulisha alipata fursa ya
kutembelea maeneo mengi ikiwa ni pamoja na makazi ya katumba na mishamo
alitoa ujumbe kule na ule ujumbe uliwafikia siyo wale tu waliohudhuria
bali pia wananchi wengine kwa sababu taarifa ile hawahusu wale tu
pekee yao .suala la kuishi kama watanzania haliwahusu wale tu pekee yake
ni pamoja na raia wengine wanaishi hapa mikoani kujua sasa tunao
raia wengine wapya 162,000 wa mkioa miwili ya katavi na tabora watambue
kuwa tuaingiliana katika maeneo mbalimbali ya maisha ya kijamii
mitaani. hivyo vyombo vy ahabari vina mchangokubwa sana.
Kwa
upande wake Meneja wa Benki ya NMB Mkoa wa Katavi Happtnes Pima
ameeleza lengo kuu la kuwatoa vifaa hivyo ambavyo ambavyo ni computer
desk top nne, printer moja na laptop moja vyote vikiwa na thamani ya
zaidi ya shilingi milioni tano za kitanzania lengo kubwa ni kuwa
benki ya nmb ni ya wananchi.
Faida
wanayoipata wanachangia na wananchi hivyo wanathamini mchango wa
waandishi wa Habari kwa sababu wanawafikia wananchi wanafanya kazi kwa
wananchi naNMB nibenki yao ,
Pimma
akaongeza katika moja ya vipaumbele vyao kwa mwaka huu ni kutoa
huduma kwa wateja ,na waandishi wa Habari nao wanatoa huduma kwa
wananchi hivyo huo ni utamaduni wa benki ya NMB.
No comments:
Post a Comment