Na Walter Mguluchuma Na Irine Temu Katavi .
Katavi yetu blog
Benki ya NMB imetowa msaada wa vifaa vitendea kazi kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi KTVPC vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milomi 5.8 vitakavyo wasaidia waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa .
Msaada huo wa vifaa hivyo ulikabidhiwa hapo jana katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi zilizopo katika mtaa wa Madukani ambapo mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga.
Awali kabla ya kukabidhi vifaa hivyo Meneja wa NMB Tawi la Mpanda Happines Pimma alieleza kuwa Benki ya NMB inatambua mchangowa waandishi wa Habari katika kuelimisha jamii.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa waandishi na kuthamini mchango wao ndio maana wameamua kutowa msaada wa vifaa vitendea kazi kwa ajiri ya chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi ili viweze kuwasaidia waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa Chama hicho .
Happiness alivitaja vitendea kazi zilivyotolewa na Banki ya NMB kwa chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kuwa ni Deski Topu Kompyuta nne Lap Topu moja na printa moja vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 5.8.
Alisema NMB imekuwa ikitowa misaada mbalimbali kwenye jamii na ndio taasisi ya Kibenki Inayoongoza hapa nchini kwa kutowa misaada mingi kwenye jamii hapa Nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga alisema kuwa msaada huo uliotolewa na Benki ya NMB kwa chama cha Waandishi wa Habari cha Mkoa wa Katavi si haba .
Alisema msaaada huo unauhakika utasaidia kupunguza tatizo la uhaba kwa vifaa vya kutendea kazi kwa Waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa chama hicho ,
Alifafanua kuwa waandishi wa Habari Mkoani Katavi wamekuwa ni chachu kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa huu kwani wamekuwa wakifikisha kwa haraka sana taarifa zinazokuwa zinatolewa na viongozi wa Serikali hasa kwenye yale maeneo ambayo viongozi wamekuwa hawafiki kwa wakati huo ila taarifa zimekuwa zikiwafikia wananchi .
Muhuga pia aliiomba NMB kuangalia uwezekano wa kukipatia vifaa vya aina nyingine chama hicho cha waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kwani yeye bado anaamini kuwa chama hicho bado ni kichanga bado hakija jitosheleza hivyo bado kinahitaji msaada zaidi .
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi Walter Mguluchuma aliishukuru NMB kwa kutowa msaada huo ambao utasaidia sana kupunguza tatizo la vitendea kazi kwa wanachama wa chama hicho .
Alisema waandishi wengi wa Habari sio wa ajiriwa bali ni wakujitegemea hivyo wamekuwa hawana uwezo wa kifedha wa kununulia vitendea kazi hivyo vifaa walivyopewa vitawasaidia kufanya kazi zao kwa urahisi na kufanya kazi kwa wingi kwa wakati mmoja tofauti na hapo awali .
Pia alitowa wito kwa Taasisi nyingine,Mashirika na watu binafsi kuiga mfano huo wa NMB kwa msaada huo waliotowa na milango iko wazi kwa chama hicho kwa kupokea msaada wa ina yoyote ile .
Nae Meya wa Manispaa ya Mji wa Mpanda Willy Mbogo aliwapongeza waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi kwa jitihada kubwa wanazofanya za kuutangaza Mkoa huo tofauti na apo awali .
Alisema yeye ni mdau mkubwa wa vyombo vya habari na amekuwa akifatilia sana kusoma magezeti kusikiliza radio na kuona Tv na kila siku zimekuwa zikitoka habari za kutoka Mkoa wa Katavi hivyo hatuna budi kuwapongeza waandishi wa Habari kwa kazi kubwa wanayo fanya .
Katika Hafra hiyo Meya huyo wa Manispaa ya Mpanda amlihaidi kulipia gharama ya kodi ya ofisi ya chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kodi ya mwezi mmoja na Mwandisi wa Tan roods Martini Mwakabende alihaidi kutowa msaada wa malipo ya mshahara ya mlinzi ya mwezi Julai.
No comments:
Post a Comment