Na Walter Mguluchuma Na Irine Temu
Katavi Yetu blog
Mgwawanyiko mkubwa umetokea ndani ya viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi hari ambayo imepelekea Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Mselemu Abdala na Katibu wa wake Everni Mushi kugawana ofisi katika maeneo tofauti huku Katibu wa CCM akiwa amehamishia ofisi yake katika chumba kilichokuwa kikitumiwa na bendi ya muziki ya Mpanda jazz .
Mgawawanyiko huo pia umesababisha kuwepo kwa makundi mawili ndani ya viongozi hao wa ngazi ya juu ambapo kundi moja linalomuunga mkono mwenyekiti huyo ni la baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa na Katibu anaungwa mkono na Sektarieti ya Mkoa huo .
Mmoja wa viongozi wa Chama hicho wa ngazi ya Mkoa ya Mkoa ambae akutaka jina lake litajwe aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa kutokana na mgawanyiko baina ya viongozi hao wawili wa ngazi ya juu wa Mkoa huu umesababisha viongoozi hao watengane kwa kugawana ofisi katika maeneo mawili tofauti aliyoko katika Mji wa Mpanda .
Alisema Mwenyekiti wa CCM yeye pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa wa Mkoa wamekuwa wakifanyia shughuli zao katika jingo linaloendelea kujengwa lililopo katika Maeneo ya Mtaa wa Majengo jirani na Posta na katibu wa CCM na Katibu wa Vijana na mchumi wa Mkoa wamehamia katika jingo la ofisi ya CCM wilaya ya Mpanda .
Kiongozi huyo alieleza kuwa viongozi hao wamekuwa na mvutano kwa kipindi cha zaidi ya miezi mine sasa huku mwenyekiti wa chama hicho akitataka ofisi yao ihamishwe kutoka Katika Mtaa wa Ilembo walikokuwa wamepanga baada ya muda wao kuwa umekwisha na wahamie katika katika jingo lao ambalo linaendelea kujengwa .
Huku Mushi akiwa yeye anataka ofisi zao zihamie kwenye jingo la ofisi ya ccm Wilaya ya Mpanda hadi hapo jingo lao la ofisi litakapo kuwa limekamilika .
Alisema hivi karibuni Mwenyekiti wa CCM Mselemu Abdala aliamuru ofisi hiyo ihamie kwenye jingo lao linaloendelea kujengwa na wakati huo Mushi akiwa safarini hari ambayo ilipelekea Katibu wa Vijana aliyekuwa anakaimu nafasi ya Katibu wa Mkoa kutokubaliana na maagizo hayo kwa kile alichodai hawezi kuhamisha ofisi wakati Katibu wa Mkoa ayupo.
Hari hiyo ilimfanya mwenyekiti wa CCM wa Mkoa aongozane na wajumbe wawili wa Kamati ya siasa ya Mkoa ambao pia ni madiwani wa Kata ya Kasokola na Mpandahotel pampja na katibu wa jumuia ya wazazi wa Mkoa na kuhamisha ofisi ya Mwenyekiti na kuhamishia kwenye jingo lao katika Mtaa wa Majengo .
Baada ya Mushi kurejea Mjini Mpanda hapo juzi na kukuta Mwenyekiti wake amehamisha ofisi yake nae aliamua hapo jana kuhamishia ofisi yake katika chumba kilichokuwa kinatumiwa na bendi ya muziki ya Mpanda jazz katika jingo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Mpanda huku akiwa anadai kuwa hawezi kuhamia kwenye jingo la ofisi ambalo mwenyekiti wake anataka wahamie wakati likiwa halina wala sakafu chini na milingo halina wala dali.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mpanda Beda Katani amelisema kuwa ametapa taarifa za kuhamia kwenye ofisi ya CCM kwa Katibu wa Mkoa kwenye jingo la Ofisi za Wilaya .
Alisema ingawa emehamia kwenye jingo hilo la Wilaya yeye kama mwenyekiti hakuwa amepata ombi lolote kutoka kwa Katibu huyo wa Mkoa .
Beda alieleza kuwa baadhi ya vifaa alivyohamishia hapo vimelazika kuhifadhiwa katika ofisi ya mchumii wa CCM wa Wilaya ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment