Na Walter Mguluchuma
Katavi
Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Katavi limepanga kuanza kutowa elimu kwenye shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Mkoa huu ili kuwafanya Wanafunzi wafahamu zaidi madhara yanatokana na Umeme .
Hayo yalisemwa hapo jana na Afisa mawasiliano na wateja wa TANESCO wa Mkoa wa Katavi Amoni Maiko wakati alpokuwa akizungumza na baadhi ya wateja wa shirika hilo katika Kijiji cha Songambele Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele waliokuwa wakililalamikia shirika hilo liwalipe fidia kutokana na hasara walioipata ya kuunguliwa na baadhi ya vifaa kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme uliotokea mei 28 mwaka huu.
Alisema watu wengi wameuzowea sana umeme ni kama vile huwa hausababishi kifo na kujisafirishia umeme bila kupitia wataalamu wa Tanesco wakati jukumu la kusafirisha na kusambaza umeme ni la Tanesco hivyo TANESCO Katavi kwa kulitambua hilo imepanga kuanza kutowa elimu kuanzia kwa Wanafunzi wanaosoma kwenye shule za Msingi na Sekondari ili waweze kufahamu madhara ya umeme wakati wangali bado wako wadogo .
Afisa huyo Mahusiano aliwaeleza wananchi hao kuwa watu waache tabia ya kupeana umeme bila kufuata taratibu kwani kufanya hivyo ni kosa na adhabu yake ni shilingi laki tano na pia wawatumia wakandarasi wanaotambulika na shirika bindi wanapokuwa wanafanya matengenezo ya umeme kwenye nyumba zao .
Akijibu swali lililoulizwa kuhusiana na kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali lililoulizwa na Lucas Maganga mkazi wa Kijiji hicho Afisa Mahusiano Amoni Maiko alisema kukatika kwa umeme kumekuwa kukisababishwa na sababu nyingine ambazo zipo nje ya shrike la Tanesco .
Alizitaja baadhi ya sababu zinazosababisha kukatika kwa umeme kuwa ni gari kugonga nguzo ya umeme , mti kuangukia kwenye waya wa umeme na wezi wanaoiba mafuta kwenye Transifoma.
Sasa hivi shirika lipo linaendelea kuwakamata watu wanaoiba umeme na limekuwa likiwapatia zawadi watu ambao wanaotowa taatifa ya kukamatwa kwa wezi na zawdi hizo
wamekuwa wakizitowa kwa usiri hivyo ni vema watu wakaendelea kutowa
ushirikiano kwa Tanesco ili kusaidia kuwabaini watu wanaoiba umeme
Nae Deo Mwaisaka Mkazi wa Kijiji hicho cha Songambelea ambao wamepata umeme hivi karibuni kupitia mpango wa Rea Yassin Nasibu aliliomba shirika la Tanesco kuwa na utaratibu wa kuwapatia elimu ya mara kwa mara wateja wake iliwaweze kuepukana na madhara kabla hayajatokea
.
Alisema watu baadhi hawana elimu na ndio maana hata wanapokuwa wamekuwa wakipata tatizo huwa hawajuwi watowe taarifa wapi .
Faustina Method alieleza kutoka na kutokuwa elimu ya kutosha kwa baadhi ya wateja wa Tanesco hasa waliopatiwa umeme wa Rea wamekuwa hawatowi taarifa kwa shirika pindi wanapotaka kuongeza ramani ya miundo mbinu yao hari ambayo imekuwa ikiwasababishia washindwe kudai haki zao pindi yatokeapo madhara ya umeme kwenye nyumba zao .
0 comments:
Post a Comment