Home » » HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA MPANDA YATOA MATAMKO MANNE

HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA MPANDA YATOA MATAMKO MANNE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
   
Na  Walter  Mguluchuma
     Katavi
  Kikao  cha  Halmashauri kuu ya CCM  Wilaya  Ya  Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  imetowa  matamko  manne  yakiwamemo  ya kuziagiza   Halmashauri  za  Wilaya ya Mpanda  na  Manispaa ya Mpanda  kukamilisha  ujenzi wa  Zahanati ifikapo Agosti 30 ilzianze kutowa huduma  kwa  wananchi  na kukifunga   kiwanda cha kusindika  mafuta kinachomilikiwa na  Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda.
Kikao  hicho  cha   Halmashauri  kuu ya  CCM  Wilaya  ya   Mpanda kilifanyika   hapo juzi  katika  ukumbi wa  Ccm   Wilaya  ya  Mpanda   kiliongozwa   na  Mwenyekiti wa  chama  hicho wa  Wliya  hiyo   Beda   Katani .
Mwenyekiti  wa  CCM  wIlaya  ya  Mpanda  Beda  Katani aliwaambia  Waandishi wa  Habari   jana  kuwa  kikao   hicho  kilitowa   matamko  manne ya kuziagiza  Halmashauri za  Wilaya ya  Mpanda  na  Manispaa  kutekeleza maazimia ya kikao  hicho .
Katani  aliyataja  maazimio hayaliyotolewa  na   kikao  hicho kwa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda ni kuwa ihakikishe   iwe imekamilisha   ujenzi wa   zahanati  katika  Kijiji cha   Kafisha   Kata ya Ikola  na  I kiwe imeanza kufanya  kazi  ifikapo  Agosti 30 iliianze kutowa huduma kwa  wananchi wanao ishi mwambao mwa  ziwa  Tanganyika .
 Pia  waliiagiza  Halmashauri  hiyo  kutowa   fedha kwa ajiri ya kiwanda cha kusindika  mafuta ya   alizeti na  karanga  cha Mpadeco vinginevyo  kama  haiwezi kufanya  hivyo ikifunge   kiwanda  hicho  kwani  akina   faida kwa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda na kwa wananchi kutokana  na kuwa na mtaji mdogo wa kukiendesha .
Mwenyekiti  huyo wa  CCM wa  Wilaya alieleza kwa  upande wa  Manispaa ya Mpanda   kikao   hicho  kimeigiza Manispaa  hiyo kuhakikisha  inakamilisha  ujenzi wa  sikimu ya  umwagiliaji ya Mwamkulu  iwe  imekamilika  ifikapo   mwezi  Novemba  mwaka huu.
Alisema  sikimu   hiyo  ambayo  ilipaswa  kuwa  imeanza  kutumiwa  na  wakulima wa  mpunga  imeshindwa  kukamilika kwa  muda  mrefu  sasa  kutokana   na  uzembe wa   mkandarasi   hivyo   chama  hakiko  tayari kuona  wananchi wanaendelea kukosa  huduma  hiyo  kwa  ajiri ya uzembe wa mkandarasi .
  Tamko  jingine walilolitowa kwa  Manispaa wameigiza   ikamilishe  ujenzi wa  ZAhanati  katika  Kijiji  cha  Mwamkuru ifikapo   mwezi wa  nane   ambapo  inajengwa kwa nguvuya  wananchi   na  Fedha za  kutoka  Tasaf  ambapo  wananchi walisha   kamilisha  mchango wao  zilizobaki  ni  fedha  za  kutoka  Tasaf.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa