Na Walter Mguluchuma
Katavi
Hari haikuwa shwari kwa zaidi ya saa moja hapo juzi katika Ofisi za Manispaa Halmashauri ya Mpanda jengo ambalo linatumiwa pia na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi baada ya waalimu zaidi ya 50 washule za Msingi na Sekondari pamoja na viongozi wa chama cha Walimu wa ngazi ya Wilaya na Mkoa kuandamana kwenda kwa mwajiri wao wakitaka walipwe ya madai yao sungu zaidi ya shilingi milioni 120.
Tukio hilo la walimu hao kuandamana hadi kwa mwajiri wao liltokea jana majira ya saanne hari ambayo ilisababisha viongozi wa Manispaa hiyo kuweza kujifisha hari ambayo iliwalazimu walimu hao kuanza kuimba nyimba kwenye makolido kwa muda wasaa nzima wimbo usemao walimu ni tegemeo la kuleta maendeleo na kufanya viongozi wa Mkoa na Manispaa kufanya kikao cha dharula na walimu hao katika ukumbi wa Manispaa kilichoongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi wa upande wa utawala Salumu Shilingi.
Mwenyekiti wa Chama cha waalimu CWT waMkoa wa Katavi John Mshota aliwasilisha madai mbalimbali ya walimu hao ambayo elieleza kuwa yamekuwa ni yamuda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi .
Mshota aliyataja madai hayo kuwa kucheleweshewa kurekebishiwa mishahara,kutolipwa fedha za nauli za likizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 kiasi cha shilingi milioni 21,848,050 ,kutolipwa gharama za masomoni shilingi milioni 25,369,700.
Madai mengine aliyataja kuwa ni kutolipwa kwa walimu wastaafu za kuwarudisha kwao kiasi cha shilingi milioni 23,839.700, gharama za uhamisho kiasi cha shilingi milioni 5,093,000,gharama za matibabu shilingi milioni 23,189,100 na fedha za chama chao cha ushirika wa kuweka na kukopa cha MPATE SACCOS shilingi milioni 24,000,000.
Mwenyekiti huyo wa CWT Mkoa wa Katavi alieleza kuwa mwajiri wao ambae ni mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ameshindwa kupeleka michango wake kwenye mfuko wa PSPF hari ambayo imewaathiri walimu wanaostaafu kulipwa malipo yao ya mafao ya kinunua mgongo kidogo na kutopewa hati zao za malipo yao ya msharahara Salary Slips za mwezi Agosti 2008.
Nae Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Mpanda Wilisoni Masolwa alieleza chama cha Walimu kilimwandikia barua mwajiri wao ya tarehe 10 machi 2016 na kumpa siku 10 yaani hadi machi 24 awe ametekeleza madai hayo lakini hadi hiyo juzi alikuwa mwajiri wao hajatekeleza wala kuwajibu majibu ya barua hiyo kwa maandishi .
Alisema ndio maana waliamua kuandamana hadi ofisini kwa mwajiri ili waweze kupatiwa majibu ya madai yao wanayodai kwa muda mrefu sasa bila kuwepo dalili za kulipwa madai hayo .
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ambae pia ni Afisa Elimu Sekondari Enelia Lungulu alikiri mbele ya walimu hao kuwepo kwa madai hayo ya walimu.
Alisema tatizo la kutolipwa kwa walimu hao halipokwao bali tatizo la kucheleweshewa kwa malipo hayo lipo hazina ambao mpaka sasa hawazituma fedha za madai ya walimu kwenye Manispaa na jitihada za mawasiliano zinaendelea kufanyika .
Lungulu alisema kuhusu fedha zao za MPATE SACCOS Kiasi cha shilingi milioni 24 ambazo zilitumiwa na manispaa hiyo wanatarajia kuzilipa hivi karibuni kwa awamu tatu .
Pia madai mengine wameshindwa kuyalipa kutokana na kiasi kidogo cha fedha zinazoletwa kwa ajiri ya kulipa walimu za likizo na matibabu .
Afisa Elimu wa Mkoa wa Katavi Ernesti Hinju alisema inaonyesha lipo tatizo baina ya manispaa na walimu kwenye swala la mawasiliano .
Alisema endapo kungekuwepo na wasiliano ya kuwajibu barua iliyokuwa imeandikwa na chama cha walimu hata hari hiyo ya walimu kuandamana isingekuwepo kwa hiyo kuwe na utaratibu wa kuwepo kwa mawasilano .
Kabla ya kuanza kikao hicho kilichochukua saa nne Katibu Tawala wa upande wa Utumishi alitaka kuwandishi wa habari watoke ndani ya kikao hicho hata hivyo walimu hao walikataa na kusema waandishi lazima wawepo ndani ya kikao hicho.

0 comments:
Post a Comment