Home » » MWENYEKITI WA KIJIJI JELA KWA KUMPIGA DAKTARI

MWENYEKITI WA KIJIJI JELA KWA KUMPIGA DAKTARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 
Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi
Mahakama  ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoa wa Katavi  imemuhukumu    Mwenyekiti wa Kijiji cha  Simbwesa    CHADEMA    Mabula  Gilede  30  kifungo  cha  miezi   sita  jela  baada ya kupatikana  na  hatia ya  kumpiga  na kumjeruhi  Daktari wa  Zahanati ya  Simbesa  Wilaya ya  Mpanda  baada ya kumtuhumu kuwa anatibu wagonjwa kwa upendeleo.
Hukumu  hiyo ilitolewa hapo  jana  na  Hakimu  Mkazi  wa  Mahakama ya  Wilaya  ya  Mpanda  Odila  Amwol   baada ya  mahakama  kulidhika  na ushahidi uliotolewa  mahakamani  hapo .
Awali  katika  kesi  hiyo  ambayo  mwenyekiti  huyo wa Kijiji  alikuwa  akitetewa na  wakil  Patrick  Mwakyusa  mwendesha  Kulwa Kusekwa  alidai kuwa  mshitakiwa  alitenda kosa  hilo  hapo   Agosti  19  mwaka  jana  majira ya saa  sita  mchana  katika  Zahanati ya  Simbwesa.
Siku  hiyo ya  tukio  mhumiwa  alidaiwa  kwenda  kwenye  Zahanati  hiyo  na kumshambuli kwa  kumpiga  mateke  na  ngumi mganga wa Zahanati  anaitwa   Razalo  Michael baada ya kumtuhumu kuwa  amekuwa akiwatibu wagonjwa kwa upendeleo kwa kuwapendelea  kuwatibu wagonjwa ambao ni wafuasi wa CCM  na kutowapatia  huduma  za  matibabu wafuasi wa  chama  chake  cha  Chadema.
 Alidai  Mahakamani kuwa  siku  hiyo ya  tukio   mtuhumiwa  kabla ya kumpiga  Daktari  huyo  ndani ya ofisi yake  wakati  akiwa  anamtibu  mgonjwa  alidai kuwa Mganga   Razaro  alikuwa  anawatibu  vibaya  wagonjwa  ambao ni wafuasi wa  Chadema  na  siku  hiyo alikataa  kumtibi  mtoto wa  rafiki  yake  aitwaye   Milembe   Machime  ambae  ni mfuasi wa  chama  chake.
Mwendesha  mashitaka   Kulwa  aliiambia  Mahakama kitendo  hicho  cha  mshitakiwa  kumshambulia  daktari  wa kumpiga ngumi  na mateke  kilisababisha  wagonjwa  waliokuwepo kwenye  zahanati  huo kushindwa kupatiwa matibabu siki hiyo kutona na  kupigwa kwa  daktari.
Katika utetezi wake  mshitakiwa   Mabula  aliiambia  Mahakama  kuwa  yeye  ndio  aliyepingwa na  Daktari huyo  hadi  aliangushwa  chini alipo  kuwa  amekwenda  kumhoji  daktati  huyo  kwa nini amekataa kumpatia  matibabu mtoto wa rafiki  yake.
Hakimu  Odira  kabla ya kusoma  hukumu  aliiambia  Mahakama  kuwa kutokana  na mwenendo  mzima wa  kesi  hiyo na ushahidi  uliotolewa  mahakamani wa  upande wa  mashitaka  mahakama pasipo  shaka   yoyote  imemwona  mshitakiwa  anayo  hatia  hivyo  kabla ya kutowa  adhabu  inatowa  nafasi kwa mshitakiwa  kama  anayosababu yoyote ya kuishawishi  mahakama  ipunguzie  adhabu .
Katika  utetezi  uliotolewa  na  Mwanasheria wake  Patricki  Mwakyusa aliomba  mahakama  impunguzie  adhabu  kwani  mshitakiwa  huyo  anao  wake  watatu na watoto 11  pamoja  na  mama  yake  mzazi  ambao wanamtegemea yeye.
 Pia  yeye  ni  mtu  anae  aminika  kwenye  jamii na  ndio maana walimchagua  kuwa  mwenyekiti wa  Kijiji na vilevile  ajawahi  kufanya  kosa   kama  hilo .
Baada  ya  maombi  hayo  mwendesha  mashitaka  Kulwa  Kusekwa alipinga na kuiomba  mahakama  itowe  adhabu kali ili  kukomesha  watu kuendelea na  tabia  hiyo .
Hakimu  Odira  aliiambia  Mahakama  wakati akisoma  hukumu  hiyo  kuwa  siku  za  hivi karibuni kumezuka  tabia ya watu kuwashambulia na kuwapiga  watumishi wa afya na kwa kuwa  mshitakiwa ni  mwenyekiti wa kijiji ameweza kufanya kosa hilo  na  inaweza ikawa  kishawishi kwa wananch kuwapiga i wa kawaida  iendapo   mahakama itamwachia huru  baada ya kupatikana  na  hatia
Hivyo  Mahakama  imemuhukumu  Razalo  Michael kutumikia  jela kifungo cha miezi  sita na kama  hajaridhika  na  hukumu  hiyo  anayo  nafasi ya kukata rufaa .
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa