Home » » ZAIDI YA KAYA 186 ZENYE WATU 596 WAMEONDOLEWA KWENYE HIFADHI ZA MISITU

ZAIDI YA KAYA 186 ZENYE WATU 596 WAMEONDOLEWA KWENYE HIFADHI ZA MISITU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Serikali  Wilayani  Mpanda  Mkoa wa Katavi imeziondoa  kaya zaidi ya 180 zenye jumla ya watu  596 ambao walikuwa wakiishi kwenye  hifadhi za mistu na kujenga nyumba  ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  aliwaambia Waandishi wa Habari jana ofisini kwake  kuwa  zoezi la  kuwahamisha watu hao  lilifanyika   kuanzia  Desemba  5 hadi  Desemba  12  mwaka huu
 Alisema   katika zoezi hilo  waliweza kushuhudia  kuwepo kwa uharifu  wa kuchungia mifugo ,  ujangili  watu kujenga nyumba  na kulima  katika maeneo tengefu
Kaya  186 zenye watu  596 wameondolewa kwenye maeneo hayo  ambapo  jumla ya vibanda  354  viliharibiwa na kuteketezwa kwa moto
Mwamlima alisema  watuhumiwa 18 walikamatwa kwenye  kwenye zoezi hilo   baada ya kupatikana na makosa mbalimbali
 Aliyataja  baadhi ya makosa waliokamatwa nayo kuwa ni kufanya ujangili  kufanya  shughuli za kilimo  kujenga ndani ya hifadhi ya Taifa  ya Katavi  kuchungia mifugo  na  kuvuna  magogo  ndani ya hifadhi  bila kuwa na kibali
Maeneo   ya hifadhi yaliokuwa yamevamiwa na watu hao  ni  msitu wa hifadhi  wa Tongwe, msitu wa hifadhi  wa Nkamba  na ushoroba  wa wanyama  wa Lyamgoroka
Mwamlima alisema kwenye zoezi hilo wamekumbana na  baadhi ya changamoto mbalimbali  katika utekelezaji wa zoezi hilo  na kuzitaja baadhi ya changamoto  kuwa ni
Uwepo  mgumu  wa kuwakamata  wahusika wa jamii ya kifugaji wenye  mifugo  na badala yake wamewakamata  watoto wadogo  wenye umri  wa miaka sita na kumi  kutokana na wazazi wao  kutokuwepo kwenye eneo husika
Changamoto nyingine ni  ufinyu wa bajeti na ushirikiano  mdogo  wa  baadhi ya viongozi  wa Kata na vijiji kutotoa ushirikiano  uliostahili
Zoezi  hilo  liliwashilikisha   Idara  za ardhi  na maliasili ,polisi , Takukuru , usalama wa Taifa  na  askari  walinzi  wa mistu  ya vijiji(VGS)

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa