Home » » DC MPANDA -VYOMBO VYA HABARI VISITUMIKE VIBAYA

DC MPANDA -VYOMBO VYA HABARI VISITUMIKE VIBAYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  amesema  kuwa  vyombo vya  habari vikitumika  vibaya  vinaweza  kusababisha   kutokea kwa machafuko  na mfarakano
Mwamlima  alitowa kauli hiyo hapo huzi  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari juzi  ofisini kwake mjini  hapa
 Alisema    kuwa vyombo vya habari   vinaumuhimu  mkubwa  sana   hivyo ni budi vishirikiane na Serikali  kwa kusaidia kuelimisha jamii
 Alieleza  vyombo vya habari  vikitumiwa vizuri  vinauwezo mkubwa wa  kuelimisha jamii  kwa haraka   hivyo  ipo haja ya  kushirikiana  kwa karibu zaidi  na Serikali  ili kutowa elimu kwa wananchi
 Hivyo   endapo  vitatumika  vibaya  upo uwezekano mkubwa  wa kusababisha  machafuko  na  mfarakano  kutokana  na watu kuwa na imani kubwa na vyombo vya habari
 Alisema  waandishi wa  habari wanao wajibu wa kuandika habari  ambazo sio za upande mmoja  kama ambavyo wanavyo fanya baadhi ya waandishi wa  habari kwa kutowa habari za upande mmoja tuu
 Alieleza ni  vizuri waandishi wa habari wakazingatia maadili yao kwa kuandika  habari  zenye ukweli  kwa kusikiliza pande zote mbili  badala ya  kutoa habari za upande mmoja tuu bila kusikiliza na upande wa pili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa