Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima ameagiza kuwa
mtu yoyote atakae ugua ugonjwa wa
kipindupindu akitibiwa na kupona atakamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka taratibu za afya
Mwamlima
alitowa agizo hilo hapo jana wakati wa uzinduzi wa usafi wa wa mazingira
na upandaji wa miti
uliofanyika katika eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo Mikoani
katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Alisema
mtu yoyote atakae ugua ugonjwa wa
kipindupindu katika Wilaya
ya Mpanda atahakikisha anapatiwa
huduma ya matibabu na baada ya kutibiwa
na kupona atakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kukiuka taratibu za afya
Mwamlima
alieleza kuwa ugonjwa wa
kipindupindu unasababishwa na
uchafu hivyo bila kuwa
na mazingira ya uchafu mtu hawezi kuugua ugonjwa huo
Alisema
ni wajibu wa kila mtu kuishi
kwenye mazingira ya usafi na wanatakiwa kupenda usafi na kuuchukia
uchafu ndio itakuwa njia pekee ya
kuepuka magonjwa ya mlipuko
Alifafanua kuwa jambo la usafi sio geni
kwani kila mtu anatambua maana ya usafi
hivyo ni vizuri kila mtu
atambua umuhimu wa usafi
Pia
Mkuu huyo wa Wilaya amepiga
marufuku baa zisifunguliwe muda
wa kazi wala watu kucheza
bao na watu kushinda kwenye vijiwe vya vinavyouza kahawa
Kwa upande Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi
amewaagiza wananchi wa
Manispaa kuhakikisha maeneo yao ya
kuishi na wanayofanyia shughuli za biashara yanakuwa katika hali ya usafi
Alisema
kila jumamosi wananchi wa
Manispaa hiyo waakikishe siku hiyo wanaitumia kwa ajiri ya kufanya
usafi kwenye mitaa yao na siku ya jumamosi ya kwanza ya mwezi itakuwa inatumika
kwa ajiri ya manispaa nzima ya Mpanda
Pia aliitaka
Manispaa hiyo kutumia sheria
ndogo ndogo za Manispaa hiyo kuwachukulia hatua watu wote ambao waeneo
yao yatabainika kuwa na uchafu
Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mpanda Hamis Mkele alieleza kuwa uzinduzi huo
wanautumia kama sehemu ya
kujitathimini katika maswala
mazima ya usafi wa mazingira
Alisema
Halmashauri hiyo ilianzishwa mwaka 2007
kama Halmashauri ya Mji na
Julai mwaka huu imepandishwa
hadhi kuwa Manispaa hivyo wameona wanalo jukumu sasa la kujipanga kwenye maswala ya usafi wa
mazingira kama Manispaa na sio kama Halmashauri ya Mji
0 comments:
Post a Comment