Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu
Vurugu kubwa zimeibuka katika mkutano wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Katavi na kusababisha kundi la wafuasi wa chama
kuwafungia mlango viongozi wao wa
Kanda , Mkoa na Wilaya wasitoke
nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kutangaza kuharishwa kwa mkutano huo
kutokana na vuurugu za wafuasi hao waliokuwa wakishinikiza baadhi ya viongozi
wao wa ngazi ya Mkoa na Wilaya wajiuzuru
Vurugu hizo zilitokea hapo jana
kwenye ukumbi wa Katavi Resort ulioko Mjini hapa
majira ya saa saba mchana
licha ya ukumbi huo kuwa umezungukwa na ulinzi wa askari wa jeshi la polisi ambao
walikuwa wapata taarifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo kuwepo kwa dalili za vurugu
Wafuasi hao na wanachama wa Chadema
wakiwemo waliokuwa wagombea wa
udiwani wa Kata mbalimbali
walianza kutowa maneno ya
kuwashutumu viongozi wao mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo na
mratibu wa Chadema wa Kanda ya
Magharibi Cristophar Namwanji
Mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo mmoja
wa wafuasi hao Shukuru alisimama
na kueleza kuwa yeye na wenzake
hawana imani na viongozi wao
kwa kuwa ni wasaliti
Kauli hiyo ambayo iliungwa mkono na kundi
kubwa ndani ya mkutano huo huku wakiwa
wanapaza sauti na kusema kuwa
viongozi hao waliwasaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kusababisha wasipate
jimbo hata moja wakati wa uchaguzi mkuu
kati ya majimbo matano yalioko Mkoani
Katavi
Mratibu wao wa Kanda ya Magharibi Namwanji
alijaribu kuwasihi wafuasi hao wawe watulivu lakini
ilishindikana hari ambayo
ilimfanya Mwenyekiti wao Kanda ya
Magharibu Mussa Masanja atoke nje ya
ukumbi na kufanya mashauriano na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mpanda Mjini ambapo walishauliana kuwa mkutano huo
uharishwe kutoka na hari ya vurugu
Masanja baada ya
kuingia ndani aliwasilisha
wazo la kuharishwa kwa mkutano huo kwa viongozi wenzake wa Kanda na mkoa
ambao wote kwa pamoja walikubaliana kuharishwa kwa mkutano huo na
walimtaka mratibu wao hawafahamishe wajumbe wa mkutano huo kuharishwa kwa mkutano
Baada ya
mratibu wao wa Kanda kutangaza
kuharishwa kwa mkutano huo kundi la
wajumbe wa mkutano huo lilianza
kupiga kelele kuwa haiwezekani na
kuwaamuru viongozi wao wasitoke nje mpaka
hapo watakapo kuwa wamejiuzuru
viongozi wanao watuhumu kusaliti
chama chao
Vurugu zilanza
ndani ya ukumbi huo wa Katavi Resort huku
milango ikiwa imefungwa kwa lengo la kuhakikisha viongozi wao
hawatoki nje ya ukumbi huo na wao
baada ya kuona hari ya usalama
wao uko hatarini waliamua kufuata matakwa ya wafuasi hao ya kuendelea na mkutano huo
Hata
hivyo kabla ya kuendelea kwa mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa
wa Katavi Laulent Mangweshi alisimama na
kuwataka waandishi wa Habari wote waliomo ndani ya ukumbi huo watoke nje hari ambayo ilipelekea wajumbe wa mkutano huo kuwanza kupiga moyowe ya kusema msiondoke msiondoke tunawahitaji muwemo huo
hata hivyo waandishi waliomua kutoka nje
Hivi
karibuni vurugu ziliibuka
katika ofisi za Chadema
Mkoa wa Katavi baada ya kundi la
wafuasi wa Chama hicho na kuwashinikiza
viongozi wao wajiuzuru kwa kuwa
waliwasaliti wakati wa uchaguzi mkuu uliopita
0 comments:
Post a Comment