Home » » HABARI YA KUSIKITISHA: AKUTWA AKIWA AMEKUFA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI AKIWA NA MPENZI WAKE

HABARI YA KUSIKITISHA: AKUTWA AKIWA AMEKUFA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI AKIWA NA MPENZI WAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mtu  mmoja  aliyefahamika kwa jina  la Livingstone   Mshiri (56)  Mkazi wa Sumbawanga  Rukwa  amekutwa  akiwa amefariki  Dunia  katika  Nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake
 Kwa  mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio  hilo  lilitokea  hapo   Novemba  saba  majira ya saa 11  alfajiri katika  nyumba ya kulala wageni inayoitwa  Manungu iliyoko  katika  Mtaa wa Majengo B    Kata ya Kashaulili  mjini  Mpanda
 Alisema  marehemu  alikutwa akiwa  amefariki  Dunia  huku  akiwa  katika   chumba  namba  nne  katika  nyumba  hiyo ya kulala wageni  akiwa chumbani  na mpenzi  wake  aitwaye   Jovina  Mathias (19)   Mkazi  wa  Kijiji  cha Mtisi  Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi
 Alifafanua  kuwa   marehemu  na  mpenzi  wake  huyo walikuwa  wamefikia  kwenye  nyumba  hiyo  ya kulala  wageni  kwa  muda wa siku  mbili
Kidavashari   alieleza kuwa  chanzo  cha  tukio  la kifo  hicho  bado  hakijajulikana  na   polisi  wanaendelea  na  uchunguzi  ili  kuweza   kubaini  chanzo   kilichopelekea kifo  cha Marehemu
 Na  jeshi  la  Polisi  Mkoa  wa  Katavi  linamshikilia  mtuhumiwa  Jovina  Mathias  ambae alikuwa  mpenzi wa marehemu  kwa mahojiano zaidi  kuhusiana na kifo  hicho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa